Rais na Waziri wa Kilimo kuhusu chakula nchini mnapotosha Taifa

Ningependa kujua huo mwaka ambao motisha ilishuka, na napenda kujua pia lini motisha ilipanda. Karibu tujadili
 
Reactions: Tsh
We hata njaa ya level one wasifunge maana tunaweza nunua nchi nyingine hata Afrika kusini nako huwa sana mahindi mengi
Hii hesabu ya wapi? Yaani uuze mahindi uliyonayo nje ya nchi, alafu ikitokea upungufu uende tena kununua nje ya nchi?
 
Ningependa kujua huo mwaka ambao motisha ilishuka, na napenda kujua pia lini motisha ilipanda. Karibu tujadili
Mkuu, Kabla ya kutaja mwaka ww ni mdau wa moja kwa moja wa kilimo? Maana kama sio utahitaji data kutoka kwenye maghala za ununuzi ambazo sitaweza kukupatia hapa. Ila kwa kukupa picha rudi kile kipindi kulikuwa na tetesi za tatizo ka korosho maghalani.
 
Mkuu, Kabla ya kutaja mwaka ww ni mdau wa moja kwa moja wa kilimo? Maana kama sio utahitaji data kutoka kwenye maghala za ununuzi ambazo sitaweza kukupatia hapa.
Mimi sio mdau tu bali ni mwekezaji mkubwa sana kwenye kilimo, nakijua vizuri sana tena kwa mazao mbalimbali. Nimekuuliza hapo uniambie lini motisha ilishuka na lini ilipanda
 
Reactions: Tsh
Mimi nimeamka asubuhi kila siku na baridi Kali kulima,ww uko barbershop ukijipodoa,nikivuna uje kunipangia pa kuuza!? Kha! Yaani wanaume wa Dar buana🚮
 
Mimi sio mdau tu bali ni mwekezaji mkubwa sana kwenye kilimo, nakijua vizuri sana tena kwa mazao mbalimbali. Nimekuuliza hapo uniambie lini motisha ilishuka na lini ilipanda
Mwekezaji mkubwa? Vizuri ww huitaji data za maghala maana lazima una maghala. Ulipeleka mazao yako nchi zipi na zipi ule mwaka ambao malori yetu yalisimama sana pale mpakani mwa kenya na Tz? Na vp serikali ilipoamua kutafuta na kuuza masoko ya mahindi moja kwa moja kama nchi kutoka kwenye maghala ya taifa kupitia control namba ilikuafect vp? Mwaka 2018 waziri mkuu alipoelekeza kuuza mahindi kwa kutoa taarifa serikalini kwanza ulifuata maelekezo? Kuna urasimu wowote ulikutana nao?
 
Kuna uongo mwingi sana kwenye huu Uzi wako. Wakulima lini waliacha kilimo?

Alafu pia bei huwa haihusiani na mipaka kufungwa wala kufunguliwa. Njoo hapa tujadili, maana naona mnaanza kulisha watu uongo. Mipaka inaweza kufunguliwa na bei ikawa chini pia.
 
Mkuu nipe data za bei kwa waliouza ghalani kuanzia msimu wa 2020 mpk leo.

Halafu ukimaliza utanieleza kati ya miaka hiyo mwaka gani umekua na mazao machache na sababu zipi zilipelekea mazao yawe machache.
 
Issue ya kwanza ilikua kuhusu motisha kushuka na kupanda, nikakuuliza ni mwaka gan motisha ulishuka na kupanda Ila hujanipa jibu, anyway...

Turudi hii issue ya pili, umesema ule mwaka malori yalikwama Kenya, ni mwaka gani? Maana hata mwaka huu pia malori yalikwama. Uwe specific kutaja mwaka ili twende sawa
 
Reactions: Tsh
Mkuu, Naomba urudie kusoma kuna maswali nimekuuliza. Ishu ya mwaka ipo wazi sana kuna jambo nataka nijue kutoka kwako kwanza ili nielewe kama kweli tutajadili au tutafanya siasa.
 
Aise viongozi wako sahihi kabisa Kama hujawahi kulima huwezi elewa acheni wakulima wajiuzie jamani Tena wauze,
 
Mkuu nipe data za bei kwa waliouza ghalani kuanzia msimu wa 2020 mpk leo.

Halafu ukimaliza utanieleza kati ya miaka hiyo mwaka gani umekua na mazao machache na sababu zipi zilipelekea mazao yawe machache.
Nimekuuliza lini wakulima waliacha kulima, hujanijibu.

Kwanza inapaswa kuniambia hapa unazungumzia mazao ya chakula au biashara. Kama ni ya chakula ni wakulima wengi hawauzii ghalani, kama ni ya biashara wala hakuna suala la mipaka maana yanalimwa ili yauzwe nje ya nchi. Turudi kweye hili la 2020

2020 mipaka haikufungwa ilikuwa wazi, Ila Bei ilikuwa chini. Na ndio sababu ya kukueleza mipaka kuwa wazi haihusiani na bei.

Aalafu unapozungumziaa uzalishaji kushuka naomba unieleze ni uzalishaji wa zao lipi?
 
Mkuu, Naomba urudie kusoma kuna maswali nimekuuliza. Ishu ya mwaka ipo wazi sana kuna jambo nataka nijue kutoka kwako kwanza ili nielewe kama kweli tutajadili au tutafanya siasa.
Umeniuliza nilipeleka mazao yangu nchi ipi na ipi ule mwaka ambao malori yalikwama. Mimi ndio nikauliza mwaka gani? Kwa maana hata mwaka huu malori yalikwama pia.

Be specific twende sawa hapa, unazungumzia mwaka gani?
 
Aise viongozi wako sahihi kabisa Kama hujawahi kulima huwezi elewa acheni wakulima wajiuzie jamani Tena wauze,
Hawa watu hawaelewi kitu, mipaka kufunguliwa haihusiani na bei kuwa juu
 
So sad endeleeni kulala wenzetu wakenya wana export hayo mazao siyo ya kula wao wanaingiza dollars sisi tumelala fofo
 
Ilo swali ulilouliza ungejibu yale niliyouliza jibu lake lilikuwepo pale tatzo hujausoma uzi Mkuu ila umeanza kusoma coment na kujibu huu uzi mzima unazungumzia mazao ya chakula hasa mahindi.

Alafu unainua NMC je wakulima hawauzi mahindi kule je unaijua TFC nayo hapo ukijua utagundua nlichoongea kwenye comment ya mwanzo uliyo quote. Ila kama ulikua mkoani Ruvuma au unafatilia habari na biashara ya mahindi Sana utajua mwaka gani uzalishaji ulipungua na mwakan gani ulipanda au ukitaka data kamili ya swali nililokuuliz tembelea NMC unaweza uliza au ukitaka data naweza leta na hiyo yote ni athari ya siasa tu.
 
Umeniuliza nilipeleka mazao yangu nchi ipi na ipi ule mwaka ambao malori yalikwama. Mimi ndio nikauliza mwaka gani? Kwa maana hata mwaka huu malori yalikwama pia.

Be specific twende sawa hapa, unazungumzia mwaka gani?
Swali si hilo tu nimekuuliza, naona unakazana na hilo la mwaka ambalo lipo wazi sana. Anyways naona tutafanya siasa.
 
Hawa watu hawaelewi kitu, mipaka kufunguliwa haihusiani na bei kuwa juu
Embu elezea hapa? Mkuu Una hakika ww ni mfanya biashara na muwekezaji mkubwa wa mazao? Mbona hili ni suala jepesi sana kwa wafanyabiashara maana pia huwa kunatabia ya kuzuia mzigo iwe michache sokoni ili bei ipande baada ya demand kuongezeka.

Unapofunga mipaka unaingilia market forces za demand and supply. Ukisema mahindi yasiuzwe nje tafsiri yake ni kuwa umesema mahindi yauzwe kwa wateja wa ndani tu ambao si wengi kama wakiwepo wa ndani na wa nje, kama watu wamevuna inamaana wateja ni wa ndani tu wanagawana mazao ambayo ni ya kutosha hapo bei lazima ishuke tofauti na ukiacha mipaka wazi wateja wa kenya na nchi nyingine wakaruhusiwa kununua unaruhusu demand kuwa juu na bei inakua juu.
 
Ukitaja mwaka shida ipo wapi? Nimekueleza wakulima wengi hawauzii ghalani, huu mbona Ni ukweli ulio wazi?
 
Swali si hilo tu nimekuuliza, naona unakazana na hilo la mwaka ambalo lipo wazi sana. Anyways naona tutafanya siasa.
Swali la mwaka ndio linadetermine jibu, ndio maana nimekuuleza hata mwaka huu malori yalikwama. Sasa hapo hujaelewa kipi?
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…