Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi
Leo naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ni aibu kwa nchi tajiri wa rasilimali kama Tanzania kuwa beggers!, ombaomba!.
Tuliambiwa tutafanya uchaguzi mkuu wetu kwa fedha za ndani, bila kutegemea fedha za wafadhili!, leo mabeberu wa ulaya EU, wamekutana na kutusingizia kuwa eti serikali yetu imewaomba mabeberu $ millioni 8 kugharimia uchaguzi wetu!, hivyo wanatupangia masherti, lazima kale ka Simba ka Kizimkazi kaachiliwe kutoka kwenye ile cage, na kundi lao waruhusiwe kushiriki uchaguzi, ndipo watupe hizo fedha!. Kama tulitangaziwa tutafanya uchaguzi wetu bila kutegemea fedha za wafadhili, halafu mijitu imekaa ulaya na kutusingizia eti tumewaomba fedha!, serikali yetu ikanushe uongo huu!. Ila kama serikali yetu ilituambia tutafanya uchaguzi bila kuwategemea wafadhili, halafu tukawaomba watusaidie, then hakuna jinsi, lazima tuu tukubali matokeo ya umasikini wetu ila tuambiwe na sio kusubiri wazungu waseme ndipo tujue kuwa kumbe sisi bado ni omba omba. Ushauri kwa serikali yetu, ikiwa kuna kitu huna uwezo nacho, hakuna ubaya kuomba kusaidiwa, ila uwe proactive kusema kabla, na sio kusubiri hadi kuaibishwa kwa kuwa ombaomba, ndipo ije kuwa reactive kuwa tuliomba!.
Kuna msemo "beggars cannot be choosers" kumaanisha ukiwa omba omba, huwezi kuchagua usaidiwe na nani na usaidiwe nini, wewe kazi yako ni kutembeza tuu bakuli kuomba tuu, chochote utakachopewa au kusaidiwa unapokea na kazi yako ni kusema tuu "hewala*, " asante". Hivyo Tanzania as beggars as we were, we had no choice but to bow down to IMF and World Bank and beg for mercy.
That was then, Nyerere aliwahi kuwakatalia Waingereza kutuingilia, wakati wa mgogoro wa Jimbo la Biafra nchini Nigeria, na akarejesha misaada yao, na kuvunja uhusiano wetu na wao wa kibalozi.
Pia Nyerere aliwahi kuwakatalia Wajerumani walipotaka kutuchagulia marafiki. Kabla ya Muungano, Tanzania ilikuwa na Ubalozi wa Ujerumani Magharibi, na Zanzibar ilikuwa na ubalozi wa Ujerumani Mashariki. Kutokana na ugomvi wao, hadi kujenga ukuta jiji la Berlin, kila watu na upande wao, nchi ikiwa na ubalozi wa nchi moja nyingine inajitoa. Hiyo tulipoungana na Zanzibar, Tanzania tukawa na balozi zote mbili, Ujerumani Magharibu wakatulazimisha kuwafukuza Ujerumani Mashariki, Nyerere aliwagomea, akawarudishia misaada yao na kuwaambia kama hawataki wao ndio waondoke.
Hata mashirika ya kibeberu ya IMF na WB, aliwakatalia kutokana na masharti yao, ila kibano kilipozidi akaamua, kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, bora ang'atuke na kupisha wengine, Mwinyi alipoingia, Ali bow down kwa kufungulia ruhsa zote.
Mambo ya Nyerere na Mashirika ya kimataifa kama World Bank, yakarejea wakati wa Rais Magufuli tangu ameingia, amebana mianya yote ya upigaji hadi vyuma vimekaza, sasa haya mashirika kwa kuanzia na WB wakaleta za kuleta kwa kutishia nyau watu wazima. Baada ya kukosa mahali popote pa kumshikia bango rais Magufuli, wakatumia baadhi ya kauli zake kama bangusilo la kutunyima mikopo.
Kama hii taarifa ya CNN eti World Bank wanatunyima mkopo wa dola Milioni 300 kuboresha elimu, kwa sababu Rais Magufuli alisema mwanafunzi atakaeshika ujauzito akiwa shule, masomo basi. Serikali yake haitasomesha.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwagomea mabeberu hawa na Mashirika yao ya kimataifa, IMF na WB, japo tuliteseka, bora tuteseke huru kuliko kulishwa tukashibishwa utumwani!. Magufuli aliwagomea na Samia asiwakubalie!
Watanzania tusimame na rais wetu, Samia, kamwe tusikubali, nchi yetu na
rais wetu kupangiwa nini cha kufanya kisa kuogopa kunyimwa mikopo na misaada yenye masharti.
Kama fedha hizo ni za kununulia makatasi ya kura, ballot papers, then tupigie kura uwanjani, watu wasimame nyuma ya mgombea, kwenye urais tuweke picha!, hawa mabeberu wakwende zao na Their blood stinking money!.
Lakini hili la nchi yetu kupangiwa nini cha kufanya ili kuwafurahisha mabeberu, tusilikubali asilan!
Mwalimu Nyerere alipowagomea IMF na World Bank, enzi zile, Tanzania tuliteseka kwa sababu tulikuwa nchi changa, nchi masikini with nothing, lakini sasa Tanzania sio changa tena, sasa Tanzania ni nchi tajiri with everything, madini, gesi asili, ardhi yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, maliasli za kutosha, watu tunao etc, hivyo hatuwezi kutishwa na yeyote kwa nchi yetu kupangiwa cha kufanya!
Hitimisho
Kwa vile Rais Nyerere na Rais Magufuli walikataa, je tumshauri Rais Samia asikubali misaada ya nchi
mabeberu, yenye masherti itakayo ingilia sovereignty yetu, au kwa vile ni sisi wenyewe ndio tumewaomba msaada wa $ milioni 8 hawa mabereru zitusaidie kwenye uchaguzi, hivyo kwa vile wenye shida ni sisi, hatuna jinsi ni lazima tujinyenyekeze tusaidiwe, na kama sherti ni ka Simba ka Kizimkazi kaachiliwe kutoka kwenye ile cage, nacho kajivinjari kwenye lile jambo letu, then kaachiliwe tuu?.
Jumatano Njema.
Paskali

Baadhi ya kauli za rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli zimeanza kutu cost kama taifa, kwa baadhi ya kauli hizo kutumika kama bangusilo la kutunyima mikopo, hivyo kuti cost na kulicost taifa. moja vya cost hizo ni hii
CNN: Tanzania loses $300m World Bank loan amid crackdown concerns - JamiiForums
Ya Mkuu Tang Zhou,
Hawa WB kama wana yao, nao ikibidi, waende zao tuu, hawawezi kutunyima mkopo wa elimu kwa kisingizio cha kauli ya Rais Magufuli kukataa mimba za utotoni. Tanzania tangu tumepata uhuru, hatujawahi kuruhusu pregnant girls kuendelea na masomo shule zile zile, alichokisema rais Magufuli sio kitu kipya, ni kuusisitiza tuu kitu kile kile kilichokuwepo miaka yote, sasa iweje hawa WB, wazuie mkopo huo muhimu sana wa elimu kwa kisingizio cha sababu hizo?!, hawa nao wana yao, kama wana yao waseme tuu, vinginevyo nao tuwafungulie tuu milango, kuwaonyesha njia ya kutokea na ikibidi kuondoka, nao waondoke tuu, kama Nyerere aliweza nchi ikiwa with nothing, Magufuli atashindwaje sasa nchi ina everything?.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwagomea mabeberu hawa na Mashirika yao ya kimataifa, IMF na WB, japo tuliteseka, bora tuteseke huru kuliko kulishwa tukashibishwa utumwani!. Magufuli aliwagomea na Samia asiwakubalie!
Bunge la ulaya laijadili Tanzania leo , lasema kama uchaguzi utafanyika na baadhi ya washiriki kuzuiliwa kushiriki kwa sababu za kisisa , eu wasitoe hata kumi kati dolla milioni 8 walizo omba tanzania kwa ajili ya uchaguzi
View attachment 3407278