Yaani nyie wafia dini mna shida. Udhaifu wa nchi za kiarabu na uimara wa israel+marekana na baadhi ta nchi za ulaya haswa german nk ndio fimbo inayawatesa waarabu. Waarabu hawana umoja. Wanawasaliti wenzao. Kwa mfano Jordan kuyatungua makombora yaliyokuwa yakadondoke israel ni usaliti kwa jumuia ya kiarabu.
Madhila na mateso wanayopata wapalestina nchi za kiarabu zilipaswa kusimama imara kuwatetea ndugu zao wa palestina. Kinyume chake woote wameufyata.
Hizbollah na houthi tu ndio wameonekana kuguswa na mateso vifo na kila baya linalowagusa wapelestina..
Kifupi tu kumshirikisha Mungu kwenye huu ugomvi ni uwendawazimu kama sio ukichaa.
Wewe ndio mfia dini.
Yaani huoni Israel ndio inayopata tabu na shida kama kondoo katikati ya mbwa Mwitu .Hivi unafikiri hao Hamasi na Hezzibolla wana nia ya kuwapa maisha bora watu au ni magaidi tu wafia dini?
Kule Somalia kuna waislam 100% na wote ni asili moja na lugha moja lakini Magaidi hawataki amani zaidi ya kumwaga damu za watu. Mpaka leo Somalia haitawaliki.
Pale Mashariki ya kati hata Israel ikiamua kuondoka bado magaidi wataendelea na vita wakitaka utawala wa itikadi wanayoitaka wao.
Magaidi hawana suluhu na mtu yeyote kutokana na kuchanganya dini na siasa na uchumi.
Tatizo sio Israel bali Magaidi wanaoungwa mkono na Irani.
Yaani huoni kuwa Nchi za kiarabu zinasaidia palestina , au huoni kuwa Urusi ,Korea ,China zinasaidia Irani na Syria ?
Yaani huoni kuwa hakuna nchi ya ulaya inayohifadhi vikundi vya kushaishambulia Palestina zaidi ya kuisaidia Israel kama Nchi nyingine marafiki?
.Hivi wewe ungekuwa ni Rais wa Israel wa Israel ungefanyaje unapoona nchi jirani inahifadhi vikundi vya ugaidi vyenye nia ya kuifuta nchi yako kwenye uso wa dunia ?
Hapa kwetu juzi tu kuna kakikundi ka watu wachache kalishiba mahindi ya kuchoma kakasema Samia must go. Wakataka tu kuandamana,nadhani uliona jinsi mkuu wa nchi alivyogeuka na kuwa mbogo huku akiviweka tayari vikosi vya ulinzi na usalama kudhibiti mitaa yote. Sembuse nchi kama Israel ukae kimya vikundi vya uasi vilipue viwanja vya ndege kwa kusaidiwa na nchi majirani kweli ? Hapo ni Udini au ni hatua za kawaida kabisa za kulinda watu wake ?
Jiulize tu na utoe jibu kichwani kwako kabla ya kumnyooshea kidole mtu mwingine
Waisrael wana mipaka wanayodai ni ya kwao kwa asili sasa kwa nini Nchi zote za kiarabu zinaamua kupoteza mamilioni ya watu kupinga hilo wakati ni kaeneo kadogo tu kasiko hata na rasilimali zaidi ya mazayuni kudai kua ni eneo lao la asili bila kujali kuwa kuna mali au laa.?
Kama nchi za kiarabu zingekuwa na nia ya kutafuta amani mashariki ya kati ingewezekana maana wanaoumia ni watu wa kawaida ambao wanaingia Israel kutafuta ajira kila siku.
Wangewekeana mipaka kwa amani na kuwasadia Wapalestina kujenga nchi yao badala ya kuwaua kwa kujitoa mhanga na kuwapa silaha. ?
Nguvu kubwa wanayoitumia kufadhili magaidi wangetumia kuijenga palestina bila shaka wananchi wa palestina wangekua na maisha bora na kushirikiana na jirani yao Israel.
Vinginevyo tubaki kwenye imani kuwa Israel ni Taifa teule la Mungu kutimiza malengo yake duniani. Na Irani inajaribu kuzuia kusudi la Mungu