Rais Putin amekubali kuuza Su-35 kwa Iran!



Wewe ndio mfia dini.

Yaani huoni Israel ndio inayopata tabu na shida kama kondoo katikati ya mbwa Mwitu .Hivi unafikiri hao Hamasi na Hezzibolla wana nia ya kuwapa maisha bora watu au ni magaidi tu wafia dini?
Kule Somalia kuna waislam 100% na wote ni asili moja na lugha moja lakini Magaidi hawataki amani zaidi ya kumwaga damu za watu. Mpaka leo Somalia haitawaliki.

Pale Mashariki ya kati hata Israel ikiamua kuondoka bado magaidi wataendelea na vita wakitaka utawala wa itikadi wanayoitaka wao.
Magaidi hawana suluhu na mtu yeyote kutokana na kuchanganya dini na siasa na uchumi.
Tatizo sio Israel bali Magaidi wanaoungwa mkono na Irani.

Yaani huoni kuwa Nchi za kiarabu zinasaidia palestina , au huoni kuwa Urusi ,Korea ,China zinasaidia Irani na Syria ?
Yaani huoni kuwa hakuna nchi ya ulaya inayohifadhi vikundi vya kushaishambulia Palestina zaidi ya kuisaidia Israel kama Nchi nyingine marafiki?
.Hivi wewe ungekuwa ni Rais wa Israel wa Israel ungefanyaje unapoona nchi jirani inahifadhi vikundi vya ugaidi vyenye nia ya kuifuta nchi yako kwenye uso wa dunia ?
Hapa kwetu juzi tu kuna kakikundi ka watu wachache kalishiba mahindi ya kuchoma kakasema Samia must go. Wakataka tu kuandamana,nadhani uliona jinsi mkuu wa nchi alivyogeuka na kuwa mbogo huku akiviweka tayari vikosi vya ulinzi na usalama kudhibiti mitaa yote. Sembuse nchi kama Israel ukae kimya vikundi vya uasi vilipue viwanja vya ndege kwa kusaidiwa na nchi majirani kweli ? Hapo ni Udini au ni hatua za kawaida kabisa za kulinda watu wake ?
Jiulize tu na utoe jibu kichwani kwako kabla ya kumnyooshea kidole mtu mwingine

Waisrael wana mipaka wanayodai ni ya kwao kwa asili sasa kwa nini Nchi zote za kiarabu zinaamua kupoteza mamilioni ya watu kupinga hilo wakati ni kaeneo kadogo tu kasiko hata na rasilimali zaidi ya mazayuni kudai kua ni eneo lao la asili bila kujali kuwa kuna mali au laa.?

Kama nchi za kiarabu zingekuwa na nia ya kutafuta amani mashariki ya kati ingewezekana maana wanaoumia ni watu wa kawaida ambao wanaingia Israel kutafuta ajira kila siku.
Wangewekeana mipaka kwa amani na kuwasadia Wapalestina kujenga nchi yao badala ya kuwaua kwa kujitoa mhanga na kuwapa silaha. ?
Nguvu kubwa wanayoitumia kufadhili magaidi wangetumia kuijenga palestina bila shaka wananchi wa palestina wangekua na maisha bora na kushirikiana na jirani yao Israel.

Vinginevyo tubaki kwenye imani kuwa Israel ni Taifa teule la Mungu kutimiza malengo yake duniani. Na Irani inajaribu kuzuia kusudi la Mungu
 
Iran kazipiga F-35 25 kwenye base mpaka leo Marekani na Israel wanaangaliana tu hawajui nini kimetokea.


Vita ya nchi na nchi sio ya kukurupuka mkuu.
Hata Tanzania tulipiga sana na Idi Amin lakini tulitulia kwanza kabla ya kutangaza vita. Kama Irani imeshambulia kwa kulipa kisasi basi ni lazima Israel nayo ijitafakari kabla ya kujibu mapigo. Maana vita haina macho .Nchi ya Israel wamejenga kwa muda mrefu hawawezi kukurupuka tu asubuhi na kuingia kwenye vita kubwa eti kwa sababu wana uwezo wa kijeshi .
Irani inamtegemea Urusi ,Korea na China kama Isarel inavyowategemea marafiki zake ,Marekani na baadhi ya Nchi za ulaya . Sasa Urusi na China kwake vita ni faida maana atauza silaha kwa nchi yenye utajiri wa mafuta. Marekani haiwezi kuruhusu Israel kuingia kwenye vita na waarabu maana mwishowe mali zake zitaathiriwa vibaya .
 
Muisrael mweusi analipoti kutoka MAKWENJE.

Mbona Gaza waliingia pamoja na kukatazwa na hao Marekani na Ulaya kwa nini Iran unaleta siasa😃
 
Iran imeshambulia Israeli, mara mbili, na shambulio kubwa zaidi la ndege isiyo na rubani katika historia na shambulio kubwa zaidi la kombora la balestiki katika historia! Israel haijajibu! Tel Aviv inajisalimisha kwa Tehran! Iran yashinda Vita!!
Imeahinda kwa sababu haijajibiwa bado au imeshinda kwamba imeutwaa mji wa tel aviv?
 
Iran imeonya mataifa ya Ghuba kwamba hatua zozote dhidi yake, ikiwa ni pamoja na matumizi ya anga au kambi zao za kijeshi na Israel, zitazingatiwa kama kitendo cha uhasama ambacho kitahitaji majibu sawia, kulingana na afisa mkuu wa Iran, kama ilivyoripotiwa na Reuters.
 
training yake sio kama ya kuendesha VITZ ....inachukuwa zaidi ya miezi 9.
 
training yake sio kama ya kuendesha VITZ ....inachukuwa zaidi ya miezi 9.
Unaleta akili za kilokole Iran, mpaka anatangaza basi fahamu mipango kaishamaliza na katoa angalizo.
Iran inatoa tishio kubwa zaidi, ikisema kwamba nchi yoyote ya Ghuba itairuhusu Israel au Marekani kutumia anga yao kwa mashambulizi ya anga dhidi ya Tehran, basi Utawala wa Kiislamu utalipiza kisasi dhidi ya mataifa YOTE ya Ghuba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…