Rais Samia aachane na mtindo wa kuhutubia njiani; hauna tija na ni hatari kwa usalama wake

Alfu mleta mada majiani ndo nini? Ni barabarani au njiani.....
 
Mnazungumzia sana demokrasia lakini naona wengi wenu mnaijuwa Domo- krasia.

Rais kuzungumzia na wapiga kura wake macho kwa macho wakiwa maeneo yao ya kuishi, na kuzungumzia kinacho wakera au nini wanataka, hicho ndio kiwango cha juu kabisa cha demokrasia, for president to physically be engaged with his constituents.

Kama anão muda aendelee tuu.
Wewe utakuwa na shida kichwani, Rais atamfuata kila mwananchi alipo? kinachotakiwa ni system nzuri kuanzia viongozi wa ngazi za chini hadi juu, ataweza kumfikia kila mtu?
 
Mwendazake ndiyo muasisi wa mtindo huu usiofaa wa kuhutubia majiani.. (naona rais SSH naye anaufanya Mwanza).

Rais anapaswa kutoa hotuba ktk eneo lililoandaliwa vema kiulinzi na kiusalama siyo kusimama majiani.

Kusimama na kuhutubia majiani ni hatari kwa usalama wa rais (rejea tukio la hivi karibuni la rais wa Ufaransa E. Macron kupigwa kibao na mwananchi).

Haya ya kusimama majiani yanawezekana kwa viongozi wanaotawala kwa mkono wa chuma (madikteta tu).

Ni ushauri tu. Mawazo hayapigwi mawe.
Kiukweli awe makini, uho utaratibu haufai
 
Majiani???????????Du !!Lugha ya wapi hii.
 
Usiogope bwana, kwani hujaliona lile gari lenye mavyuma vyuma kwa juu? Si linampa ulinzi?
 
Hivi kama raisi hasimami sehem akasikia matatizo ya wananchi wake kupitia vinywa vyao wenyewe atajuaje kama wananchi hao wanashida ya maji, barabara, umeme na kero nyingine nyingi zinazowahusu wananchi wa sehem husika. Kumbuka wawakikilishi wengi wa wananchi wakiwemo wabunge, huwa wanawakilisha tu matatizo ya matumbo yao ili waweze kuongezewa mishahara yao.
Huu nao ni mtazamo wako. Wacha tuuheshimu
 
Mwendazake ndiyo muasisi wa mtindo huu usiofaa wa kuhutubia majiani.. (naona rais SSH naye anaufanya Mwanza).

Rais anapaswa kutoa hotuba ktk eneo lililoandaliwa vema kiulinzi na kiusalama siyo kusimama majiani.

Kusimama na kuhutubia majiani ni hatari kwa usalama wa rais (rejea tukio la hivi karibuni la rais wa Ufaransa E. Macron kupigwa kibao na mwananchi).

Haya ya kusimama majiani yanawezekana kwa viongozi wanaotawala kwa mkono wa chuma (madikteta tu).

Ni ushauri tu. Mawazo hayapigwi mawe.

Hivi wewe Ni Nani hasa . Umekuwa lini mshauri wa Rais. JPM amekwisha kwenda. Lini mtaacha kuhangaika na kuteseka na marehemu.
 
Mwendazake alitesa, aliteka na kuuwa. Ndiyo maana bado tunamsimanga ili ateswe vizuri huko motoni.
 
Muacheni SSH aongoze nchi, acheni kumhujumu raisi, watanzania watu wabaya sana..
 
Pale mahali kuna maaskari wa kila aina. Mwanza ni kwa JPM ambaye ndio aliyempa umakamu uliompa fursa ya urais.

Nilichogundua ni kwamba huwa anakohoa akisimama na kuhutubia akiwa garini.

Wasukuma wanapenda sana kuonyesha kwamba wapo. Tena kwa kutumia nguvu nyingi sana.😂😂😂😂😀
 
Hivi kama raisi hasimami sehem akasikia matatizo ya wananchi wake kupitia vinywa vyao wenyewe atajuaje kama wananchi hao wanashida ya maji, barabara, umeme na kero nyingine nyingi zinazowahusu wananchi wa sehem husika. Kumbuka wawakikilishi wengi wa wananchi wakiwemo wabunge, huwa wanawakilisha tu matatizo ya matumbo yao ili waweze kuongezewa mishahara yao.
Kweli kwa dakika 10-30 anazosimama barabarani anaweza KUFAHAMU shida za wananchi? Vipi wale ambao hawapati fursa ya kuzungumza? Vipi wale walio mbali kama kule Nyambiti, Ng'washilalage, Ng'wabaghole n.k.?

Pili, kama Rais anasubiria kujua kero za wananchi kupitia hizo rapid assessments, huoni kama ni tatizo katika mfumo wa mipango na sera?

Na mwisho, hivi kuna kero au shida ambayo haijulikani (mpya) mpaka Rais asimame barabarani?
 
Back
Top Bottom