Rais Samia aachane na mtindo wa kuhutubia njiani; hauna tija na ni hatari kwa usalama wake

Rais Samia aachane na mtindo wa kuhutubia njiani; hauna tija na ni hatari kwa usalama wake

Mwacheni Madam ahutubie
Halafu mbona kumpangia sana maisha aiseh??
Mwacheni afanye kazi subiri 2030
Kukohoa sio dhambi ni dalili ya mtu mwenye Afya
Mwacheni apumzike madame apige kazi
Kweli kabisa
 
Hivi kama raisi hasimami sehem akasikia matatizo ya wananchi wake kupitia vinywa vyao wenyewe atajuaje kama wananchi hao wanashida ya maji, barabara, umeme na kero nyingine nyingi zinazowahusu wananchi wa sehem husika. Kumbuka wawakikilishi wengi wa wananchi wakiwemo wabunge, huwa wanawakilisha tu matatizo ya matumbo yao ili waweze kuongezewa mishahara yao.
Hamna haja ya yeye kusimama. Leo kasimama anatokea mmama ana duluduku lake anataka aongee na rais moja kwa moja yeye anasema muacheni aongee na maofisa wangu....asiwe anasimama basi...hao maofisa ndio wamesababisha dukuduku lake lisigike kwake kabla sasa mmama kaiona fursa ya kuongea nae moja kwa moja yeye anampeleka kwa maofisa wake
 
Mwendazake ndiyo muasisi wa mtindo huu usiofaa wa kuhutubia njiani.. (naona Rais Samia naye anaufanya Mwanza).

Rais anapaswa kutoa hotuba kaatika eneo lililoandaliwa vema kiulinzi na kiusalama siyo kusimama majiani.

Kusimama na kuhutubia njiani ni hatari kwa usalama wa rais (rejea tukio la hivi karibuni la rais wa Ufaransa E. Macron kupigwa kibao na mwananchi).

Haya ya kusimama njiani yanawezekana kwa viongozi wanaotawala kwa mkono wa chuma (madikteta tu).

Ni ushauri tu. Mawazo hayapigwi mawe.

Sasa kama Rais Magufuli alikuwa dictator kama mnavyodai,aliwezaje kupenyeza kwenye makundi ya watu na kusikiliza shida zao bila uoga wowote na bila kudhulika? leo hii huyu sio dictator na bado mnahofia usalama wake?
Unafikiri JPM alikuwa mjinga kuanzisha utaratibu huu?kati ya mwananchi na mteule wake unafikiri ni upande upi unaweza kutoa taarifa sahihi na za kweli?
 
Mwendazake ndiyo muasisi wa mtindo huu usiofaa wa kuhutubia njiani.. (naona Rais Samia naye anaufanya Mwanza).

Rais anapaswa kutoa hotuba kaatika eneo lililoandaliwa vema kiulinzi na kiusalama siyo kusimama majiani.

Kusimama na kuhutubia njiani ni hatari kwa usalama wa rais (rejea tukio la hivi karibuni la rais wa Ufaransa E. Macron kupigwa kibao na mwananchi).

Haya ya kusimama njiani yanawezekana kwa viongozi wanaotawala kwa mkono wa chuma (madikteta tu).

Ni ushauri tu. Mawazo hayapigwi mawe.

Wafanyeje Sasa kama Wananchi wamewasimamisha😆😃😋
Kwa kuwaWatanzania wanauwezo was kuusimamisha msafara was Rais!🙄🙄🙄
 
Naunga mkono hoja, huyu mama akifa Mpango anaapishwa chonde chonde jamani tafadhali tunaomba mumlinde huyo mama, wengine ingawa tuna njaa tukimuona tunajisikia kushiba.
 
Mwendazake ndiyo muasisi wa mtindo huu usiofaa wa kuhutubia njiani (naona Rais Samia naye anaufanya Mwanza).

Rais anapaswa kutoa hotuba kaatika eneo lililoandaliwa vema kiulinzi na kiusalama siyo kusimama majiani.

Kusimama na kuhutubia njiani ni hatari kwa usalama wa rais (rejea tukio la hivi karibuni la rais wa Ufaransa E. Macron kupigwa kibao na mwananchi).

Haya ya kusimama njiani yanawezekana kwa viongozi wanaotawala kwa mkono wa chuma (madikteta tu).

Ni ushauri tu. Mawazo hayapigwi mawe.

Pole sana blazaaa...hatukukushauri kuwa na cheti feki..ila ndo maishaaa songa mbelee..jitahd kutafuta riziki kwa njia halali
 
Back
Top Bottom