Rais Samia aachane na mtindo wa kuhutubia njiani; hauna tija na ni hatari kwa usalama wake

Alfu mleta mada majiani ndo nini? Ni barabarani au njiani.....
 
Wewe utakuwa na shida kichwani, Rais atamfuata kila mwananchi alipo? kinachotakiwa ni system nzuri kuanzia viongozi wa ngazi za chini hadi juu, ataweza kumfikia kila mtu?
 
Kiukweli awe makini, uho utaratibu haufai
 
Majiani???????????Du !!Lugha ya wapi hii.
 
Usiogope bwana, kwani hujaliona lile gari lenye mavyuma vyuma kwa juu? Si linampa ulinzi?
 
Huu nao ni mtazamo wako. Wacha tuuheshimu
 

Hivi wewe Ni Nani hasa . Umekuwa lini mshauri wa Rais. JPM amekwisha kwenda. Lini mtaacha kuhangaika na kuteseka na marehemu.
 
Hivi wewe Ni Nani hasa . Umekuwa lini mshauri wa Rais. JPM amekwisha kwenda. Lini mtaacha kuhangaika na kuteseka na marehemu.
Mwendazake alitesa, aliteka na kuuwa. Ndiyo maana bado tunamsimanga ili ateswe vizuri huko motoni.
 
Muacheni SSH aongoze nchi, acheni kumhujumu raisi, watanzania watu wabaya sana..
 
Pale mahali kuna maaskari wa kila aina. Mwanza ni kwa JPM ambaye ndio aliyempa umakamu uliompa fursa ya urais.

Nilichogundua ni kwamba huwa anakohoa akisimama na kuhutubia akiwa garini.

Wasukuma wanapenda sana kuonyesha kwamba wapo. Tena kwa kutumia nguvu nyingi sana.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜€
 
Kweli kwa dakika 10-30 anazosimama barabarani anaweza KUFAHAMU shida za wananchi? Vipi wale ambao hawapati fursa ya kuzungumza? Vipi wale walio mbali kama kule Nyambiti, Ng'washilalage, Ng'wabaghole n.k.?

Pili, kama Rais anasubiria kujua kero za wananchi kupitia hizo rapid assessments, huoni kama ni tatizo katika mfumo wa mipango na sera?

Na mwisho, hivi kuna kero au shida ambayo haijulikani (mpya) mpaka Rais asimame barabarani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…