Rais Samia aachane na mtindo wa kuhutubia njiani; hauna tija na ni hatari kwa usalama wake

Wewe ndio msemaji wa watu?
Alionekana tu. Kwani kuna mtu alikuwa hajui hilo? Kilichomuua unakijua? Alitumia nguvu sana kutafuta sifa mpk akapungukiwa kinga, akashambuliwa na korona ikakata moto wa pacemaker.
 
Umedhiirisha hoja yangu; kuna tatizo kwenye mfumo wa utendaji kazi. Nchi hii ilivyo kubwa kutegemea mpaka Rais apite ndiyo tatizo litatuliwe, hakuna ufanisi hapo.
 
Msimpangie Mama.. Lipi jema kwenu?
 
Wananchi wangapi wanapata fursa ya kutoa kero zinazowasibu kwenye hiyo mikutano isiyo rasmi ya njiani?
Wananchi wangapi wanapata shida kutokana na kero ya mikutano isiyo rasmi ya njiani!?
 
Umedhiirisha hoja yangu; kuna tatizo kwenye mfumo wa utendaji kazi. Nchi hii ilivyo kubwa kutegemea mpaka Rais apite ndiyo tatizo litatuliwe, hakuna ufanisi hapo.
Mkuu.. ndio maana nikasema raisi na serikali yake ni binadam kama tulivyo mimi na ww. Hawawezi kujua kila linalofanyika nchini bila mengine kuyaona au kuyasikia wenyewe kutoka kwa wahusika. Hata marekani ambapo wengi tunaamini kwamb wana mifumo imara kuna mambo mengine huwa yanafanyika bila serikali au raisi kujua, chukulia mfano swala la Urusi kuingilia uchaguzi wa marekani mwaka 2015 chini ya raisi Obama, walifanya kile walichofanya bila Obama mwenyew au serikali yake kujua japo walikuja kujua baadae kabisa baada ya uchaguzi kumalizika, wahamiaji haramu wanaingizwa marekani kupitia njia za panya na vyombo vya usalama wakishirikiana na uhamiaji vipo, Oliega alikuwa muingizaji na muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya lkn ilichukua miaka mingi bila vyombo vya usalama kumkamata nk. Kwahiyo kuna mambo au kero nyingine haziwezi kutatuliwa ki urahisi mpk pale mkubwa anapoingilia kati kwa vile hawa wa chini wengi (sio wote) ni wababaishaji na ubabaishaji haupo kwa Tanzania pekee bali ni kwa dunia nzima kama nilivyokutolea mfano hapo juu. Ni Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kujua kila kinachofanyika hapa dunia iwe usiku au mchana.
 
Utetezi dhaifu, wawakilishi wote kuanzia serikali za mitaa, madiwani mpaka wabunge ni wa ccm, ni kero zipi wameshindwa kumpelekea mpaka yeye awasikie hao wananchi mwenyewe? Huyo mama anachofanya ni copy & paste zile mbinu ya siasa za Magufuli akidhani ndio zitaipa ccm mvuto.
 
Samia amekwisha kataa kuona kero za watu kwenye mabango, je anaruhusu kusikia kero hizo hizo kwa mdomo?
Bango linaweza kuandikwa hata matusi na mbebaji akadai kwamb alipewa na mtu akaliwakilishe huku yeye mwenyewe mbebaji akiwa hajui kilichoandikwa maana hajui kusoma wala kuandika. Lkn matusi hayo ya kwenye bango mtu hawezi kuyaongea kwa kinywa chake mwenyew afu aseme eti alikuwa haelewi anachoongea.
 
Ndio maana wachumia tumbo na wafia upinzani wengi wanaonesha kukerwa na style hii, maana wanajua ndio itakuwa kaburi lao mwaka 2025 baada ya muheshimiwa raisi kujua kero na matatizo ya wananchi kupitia njia hii na kuzitatua kwa wakati. Tuliona viongozi wengi wali copy hii style ktk uchaguzi wa mwaka 2020 mmoja wao ni Lisu alipokuwa anasimama na yeye njiani kujifanya ana wasalimu wananchi na huku akipiga kampeni zake hapo hapo. Kuendelea kutumiwa na wanasiasa chakavu wa upinzani kama daraja la kufikia mipango yao inataka moyo aisee.
 

Mahindi ya kuchoma hayakuwepo hapo?
 

Nimecheka kwa nguvu, eti ndio njia ya kutatua kero, kama wawakilishi wote wa wananchi wameshurutisha kuwa wanaccm ashindwe kutatua hizo kero, ndio ataweza kutatua kwa kuleta jam barabarani?

Lisu alisimama wakati wa kampeni, tena wakati huo wapinzani walikuwa hawaruhusiwi kufanya siasa nchi nzima. Je ccm wana ufinyu gani wa kufanya siasa hadi asikilize kero kijima?
 
Yaani hamtaki afanye,kisa jpm alifanya..hahhhaaa huu mtindu haukuasisiwa na jpm weka kumbukumbu zako vizuri
 
Mama anapita njia za meko,yeye kila uchwao ni kuzindua vitu ambayo waziri anavimudu,angejikita kufanya marekebisho angalia budget ilivyo ya hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…