Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Uwe unatumia akili kwahiyo na waliowaajiri nao , na waliowathibitisha kazini nao washtakiwe ? . Tumia akili roho mbaya weka pembeni .
Huna Akili hata kidogo,mlipeleka vyeti feki tunaanzia hapo mlipwe haki yenu then tuwapeleke kortini kwa kughushi.
 
Watanzania uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo sana na morals zetu ni very low.Sawa umefanya kazi,lakini si ulidanganya in the first place na ulijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Sasa kwa kuwa umefanya kazi kosa la kugushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu linapotea!Ajabu sana.Hivi kwa nini mnatetea uovu?

Ningekuwa Mama Samia ningesema mlipwe haki zenu,ila mpelekwe mahakamani kwa kosa la kugushi vyeti na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
 
Mkuu wenye mentality zilizojaa roho mbaya ni wale wenye elimu za kuunga unga walizopata kwenye vyuo vya uchochoroni, mtu mwenye elimu ya kueleweka huwezi kufurahia kunyanga'anywa stahiki za mtu aliyefanya kazi miaka yote na kazi zake kukubalika kwamba zinakidhi matarajio ya mwajiri..
 
Tatizo la vyeti feki lina sura mbili walioajili na walioajiliwa wote walitakiwa kuadhibiwa
 
Shida sana.
 
Watanzania uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo sana.Sawa umefanya kazi,lakini ulidanganya in the first place.Sawa kwa kuwa umeganya kazi kosa la kugushi na kuibia serikali linapotea!Ajabu sana.
Kuna kosa la kugushi cheti, lakini nimezungumzia wale waliosoma kwa majina ya watu wengine, wakahitimu wakaajiriwa, wakafanya kazi kwa jasho lao, wameibia nani?! Halafu Watanzania na Waafrica kwa ujumla tu ndo makaratasi (vyeti) yanapewa kipaumbele kuliko ujuzi! Kuna wasomi wangapi wamesoma kwa majina yao wana vyeti halali, lakini walinunua mitihani, wamesoma na kufaulu kwa rushwa! Profesa Assad alisema 60% ya watumishi wa uma siyo compitants katika kazi wanazofanya! Wewe inalilia cheti tu? Kuna wenye vyeti wapo kazini, wanalipwa lakini hawafanyi kazi kwa ufanisi!
 
Kama ulifanya kazi kwa jasho na ukachangia mifuko,lazima ulipwe,hatutaki dhulumati dhulumati
Cheti feki alifanya kazi gani? ya kumdhulumu mwenye cheti halali asipte haki yake ya kuajiriwa akae yeye?

Vyeti feki wanatakiwa kurudisha pesa zote toka tarehe ya kwanza waliyoajiriwa ni wahujumu uchumi na wezi wa mali ya umma kwa njia ya udanganyifu serikali inatakiwa itaifishe hadi mali zao ziwe pensheni au chochote
 
Nashukuru mkuu! Kuna jamaa amereply kama mawazo yangu ni potofu, ameponda na Watanzania kwamba tuna uwezo mdogo wa kuelewa! Inawezekana ndo hao wenye elimu za kuunga unga’
 
Usitake ku pick and choose. Kama unataka sheria ifuatwe, ifuatwe yote na si kwa baadhi ya kundi la watu. Kwa hiyo taka kujua.

Sheria inapotekelezwa kwa baadhi ya watu, wengine wanaachwa, inakuwa uonevu.
 
Mimi sija-ungaunga elimu yangu lakini siungi mkono swala hilo.Mtu aliye-gushi cheti na kufanya kazi amefanya makosa mawili:
1.Kugushi cheti,kosa ambalo ni prosecutable by law,
2.Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa ambalo pia ni prosecutable by law.

Sasa tuwe wakweli tu, mtu kama huyo ana lipwaje mafao,si alitakiwa kupelekwa mahakamani in the first place.

Kiukweli maamuzi ya kuwalipa hawa watu hayaja-zingatia sheria,weledi na yana-set an extremely bad precedent.

Tunaomba Rais afikirie upya maamuzi yake,yanachangia moja kwa moja katika kuiharibu jamii yetu morally.
 
Wakirudisha pesa walizo lipwa, Wewe utairudishaje kazi waliyo fanya? Yalikua malipo ya cheti au ya kazi?
Haiwezekani eti kwa kuwa Wewe ni mwabudu jiwe, basi kila dhuluma ihalalishwe kisa tu msimamo na imani zenu potofu! Penda usipende Mazaa ameamua, WALIPWE!
 
Kuna kosa la kugushi cheti, lakini nimezungumzia wale waliosoma kwa majina ya watu wengine, wakahitimu wakaajiriwa, wakafanya kazi kwa jasho lao, wameibia nani?!
Hapa kuna kituko kikubwa tu unakuta mfano Asha Mataputapu alisoma chuo cha ualimu

Cheti hicho hicho unakuta kuna walimu 10 wameajiriwa sehemu mbali mbali kwa jina hilo hilo la Asha mataputapu

Ukiwambia lete cheti cha form four original wanakuwa hawana anacho mmoja tu.

Wengine alikuwa akiomba kazi yeye anampa ndugu yake darasa la saba akaombee kazi cheti hicho hicho .Ilipofika uhakiki huyu mwingine akiomba cheti original nduguye kuwa nipe na mimi kikahakikiwe nduguye anaogopa jela au kufukuzwa kazi sababu kitaonekana mara ya pili

Waathirika wakubwa wa kupeana vyeti wengi walitoka mikoa miwili ya watu wanaojifanya wajanja sana nchini
 
Sheria zipo kwa ajili ya binadamu sio binadamu kwa ajili ya sheria, ndo maana huwa tunahalalisha misamaha ya raisi baada ya hukumu.
Usiongozwe na roho ya aina hiyo, haitakupeleka popote katika siku zako za kuishi.
Uongo vinginevyo hata mama Samia asingekuwa Raisi Wahuni wangemgomea.Sheria ndizo zimemuweka pale
 
Nashukuru mkuu! Kuna jamaa amereply kama mawazo yangu ni potofu, ameponda na Watanzania kwamba tuna uwezo mdogo wa kuelewa! Inawezekana ndo hao wenye elimu za kuunga unga’
Mkuu jikite kwenye hoja ukianza ukianza kutaja Elimu za watu watakuja wa Stellenbosch UN wewe na mimi na kayumba zetu tutakimbia niliwahi ulizwa eti chuo kikuuu Tanzania kipo ambacho kina uhaba wa maji au stationery za chuo wananunua nje ya chuo hawatengenezi wao...
 
Kosa la kudanganya na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lipo pale pale mkuu.Umepata fedha kwa njia ya udanganyifu!And than mambo mengine ni ya ajabu sana,wewe una-matatizo gani mpaka utumie cheti cha mtu mwingine?Mwenzio kasoma mpaka kafika point X ,halafu wewe unadandia juu kwa juu,huoni kwamba hilo ni kosa!

Nirudie,Watanzania inabidi tubadilike,our moral values are way too low.
 
Kosa namba 2 linakuaje kama alifanya kazi? Cheti ni kikatatasi tu, hata cha kwako kwa hapa hakikusaidii kufikiri vizuri!
Suala la msingi, mama ameamua walipwe na maumivu yenu yapo kwenye maamuzi ya mama kwenda kinyume na #yesuwalugola wenu! Legacy legacy, legacy! na mengi yatapanguliwa na madudu kuibuliwa!
 
Mwalimu asiye na cheti cha ualimu alifanya kazi gani ya maana? WAtoto walikuwa wakimaliza shule za msingi wengi hawajui kusoma wala kuandika kwa sababu yao

Utendaji maofisini ulijaa ubabaishaji sababu ya hiyo mijitu ya vyeti feki

Sasa hivi wenye vyeti halali wameshika nafasi ufaulu uko juu na nenda maofisini baada ya mijitu yenye vyeti feki kuondoka huduma ziko vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…