Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Huyu nina wasi wasi hata yeye ana vyeti feki sasa anakuja kutafuta sympathy. Anyways kakosea platform labda aende Facebook huko ndipo wapo watu wa ajabu kama yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna platform yenye watu wa ajabu. Ww kuwepo JF hakukupi upekee wa aina yoyote. 🤣. Ushawishi wa hoja ndo kipimo cha kufanya mtu akubaliane na ww au apingane na wewe. Si aina ya platform unayotumia.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Shida ni mfumo wa ajira ulikuwa mbovu na usio makini hivyo ulipelekea watu kuingia kwenye ajira kirahisi bila kuwa na vigezo. Hivyo lawama ni kwa serikali na kwa wote walioingia kwenye utumishi wa uma kwa udanganyifu. Mh Rais kama anawalipa ni vema kwa sababu mfumo uliruhusu udanganyifu
 
Ukiitwa kuthibitisha utwezana ?
Mbona jeshini , polisi , magereza , uhamiaji na usalama wataifa hawakufukuzwa kazi huko jeshini cheti kimoja mpaka watu kumi wanakitumia na Wana vyeo vikubwa sana , hii double standard ya nini ?
 
Muwe mnaelewa!!sio kukurupuka tu!!hakuna aliposema darasa la saba wenye vyeti feki walipwe, darasa la saba wote walioajiriwa baada ya 2004, na kushindwa kujiendeleza ndio waliondolewa kazini, lakini walioajiriwa kabla ya 2004, wakati sheria haijabadirika hata kama hawakujiendeleza walibakia kazini, ila wengi wao mwaka jana ndio wamestafishwa mimi nina mfano wa watu wawili nawafahamu, ndio amewazungumzia hao kuwa wanatakiwa kulipwa mafao yao!kwani serikali ilikuwa bado haijatoa muongozo, na mwendazake, alikuwa hajaamua, kuwa walipwe au vipi!!Hivyo wana haki kama watumishi wengine, tatizo ninalo liona huu ni mzigo mkubwa sana kwa serikali kwani wengi walikuwa wamebakiza miaka 1, 2, 3, 4 sasa karibia wote unawastafisha kwa wakati mmoja,?!!ndio maana meko baada ya kuona ameshabugi, aka waweka pending kwanza!!!
Wala hakubugi. Alifanya kazi yake vizuri tu.
 
Kumbe hujui nyumbu wa lile li chama la kaskazini ndio wengi waliopigwa chini kwa vyeti fake
Watanzania wengi elimu hamna. Na hata wale waliosoma majority yao elimu haina msaada katika upande wa upeo.

Imagine mtu analaumu serikali kumdhibiti mtu aliyefoji vyeti kupata kazi, eti na yeye anapiga kelele huyu mtu kulipwa stahiki!

Kiukweli hii ni aibu kubwa sana katika taifa kuwa na raia ambao wanaamini hisia ndio muamuzi wa hatima ya taifa badala ya sheria, kanuni na taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio yeye atakayefunga watu 1000 wala mimi kupata kitu chochote,hiyo ni sheria kufuata mkondo mkuu,wapewe haki yao ya mafao ila tusiishie hapo kama walighushi na sheria ina maelekezo yake kwa mtu aliyeghushi,nao ufuatwe halikadhalika.
Na sheria hii itekelezwe kwa kada zote zilizopo kwenye ajira ya serikali, nikimaanisha ijumuishe vyombo vya usalama na ajira za kisiasa. Sawa?
 
Shida ni mfumo wa ajira ulikuwa mbovu na usio makini hivyo ulipelekea watu kuingia kwenye ajira kirahisi bila kuwa na vigezo. Hivyo lawama ni kwa serikali na kwa wote walioingia kwenye utumishi wa uma kwa udanganyifu. Mh Rais kama anawalipa ni vema kwa sababu mfumo uliruhusu udanganyifu
Mfumo haukuruhusu udanganyifu bali watu walitumia mfumo dhaifu wa serikali kuidanganya serikali.......kwa lugha nyepesi hao ni matapeli.....wameitapeli serikali kwa kipindi chote walichokuwa wanatumikia......hata huo mshahara waliokuwa wanapokea ni haramu kwa maana waliopokea hali ya kuwa wanajua kuwa wanatumia udanganyifu.......hivyo basi hata makato yaliyotokana na huo mshahara ni haramu.......wao ndio wanatakiwa wailipe serikali mishahara yote iliyokuwa inawalipa......kwenye zinazoongozwa kwa utawala wa sheria walitakiwa wawe jela muda huu.......
 
Hili la vyeti fake halikuchukuliwa kwa umakini bali lilifanywa kuridhisha yule mzee,, maana akisema halafu ukafanya tofauti hata kam ni kwa weledi alikuwa anakufukuza kazi, anakufunga au unatumiwa wasiojulikana.
Hebu fikiria ,,kuna maprofesa waliambiwa wana vyeti fake.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Uchunguzi ufanyike na wanaostahili wapate wanachostahili.....lakini kuwalipa waliotumia vyeti feki ni haramu......
 
Kuna kitu kinaitwa kisheria "due diligence" ambapo mwajiri alipaswa kisheria kujirudhisha kabla ya kumwajiri mtu,kama hilo halikufanyika then wote mwajiri na mwajiriwa ni wahalifu tu,hivyo mama Samia amekuja na balancing decision kuwa walichochangia kwenye mifuko ya kihifadhi ya jamii walipwe tu iwe bye bye basi.Usikute kulikuwa na corrupt system ya kuajiri in those days ,sasa hapa hakuna anayepaswa kutema huu mzigo
Wanaochapisha fedha bandia wanajitahidi kuifanya ifanane na fedha halali.....na hatimaye kuingia kwenye mzunguko wa fedha kwa watu kushindwa kuitambua mapema......lakini kushindwa kuitambua kwa anayepewa na kuitumia haimaanishi kuwa fedha hiyo ni halali.....
 
Watanzania wengi elimu hamna. Na hata wale waliosoma majority yao elimu haina msaada katika upande wa upeo.

Imagine mtu analaumu serikali kumdhibiti mtu aliyefoji vyeti kupata kazi, eti na yeye anapiga kelele huyu mtu kulipwa stahiki!

Kiukweli hii ni aibu kubwa sana katika taifa kuwa na raia ambao wanaamini hisia ndio muamuzi wa hatima ya taifa badala ya sheria, kanuni na taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili sio suala la elimu ni suala la uzalendo kwa nchi yako.....waTanzania walio wengi ni wahalifu wanaongoja kupata nafasi ya kufanya uhalifu.....hii mentality imeathiri kwa kiasi kikubwa sana kwenye jamii zetu kiasi kwamba uhalifu limekuwa jambo la kawaida kwenye macho ya wanajamii......Hakuna anayewapa credit wachapakazi bali wahalifu ndio wanaopewa heshima.....

HAO WANAO TETEA HAO WAHALIFU KULIPWA NDIO ZAO LA WANAJAMII HIYO HIYO.....
 
Hongera Rais , kwa kuamua kulipa haki zao stahiki Mungu akubaliki sana . Katika hotuba yake leo amesema watumishi wa darasa la na vyeti feki walikuwa wakichangia mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo amewataka waajiri wote kuhitimisha utumishi wao kwa kuwalipa stahiki zao . Sikikiza hotuba yake dakika ya 13 mpaka 16 .View attachment 1770203
Kisheria hawatakiwi kulipwa,kwa sababu walipata hiyo mishahara kwa kugushi,hawa inabidi washitakiwe.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Kuna mabwege watachekelea wakidhani watalipwa kweli!😂😂😂
 
Kama ulifanya kazi kwa jasho na ukachangia mifuko,lazima ulipwe,hatutaki dhulumati dhulumati
Kazi kwa dhati kwa kugushi vyeti!kugushi ni kosa la jinai.
Mtu akikuibia gari yako,akaitumia kama gari la wagonjwa,au akafanyia biashara na akawa ana hudumia watoto yatima,siku ukimkamata akakuambia aliiba lakini alifanyia mema,kwahiyo yale mapato ni ya Kwake,utajisikiaje?
 
  • Thanks
Reactions: R.K
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Kama mnaweledi mbona tiss, jwtz, polisi, uhamiaji magereza mbona hamkuwaguza
Wakati huko ndiko wapo wengi kuliko sekta zote.?
Acheni double standard
?
 
Back
Top Bottom