Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....
Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........
Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Kuna mambi mengi yanayoweza kusababisha mtu kuamua kutumia busara badala ya sheria:
1: Historia ya elimu yetu hapo zamani ilitoa mwanya wa mtu kurudia shule kwa kutumia jina la mtu mwingine, japo si kisheria. Msingi wa majina kutofanana, kwa kutumia hii huko serikalini ni mafuriko hasa wasomi wa siku nyingi.
2: Kutokuwa makini wakati tunajiandikisha kwenye tasisi tofauti kwa kuwa watu hawakujua kama haya yatakuja kutokea.
3: Zoezi lilivyoendeshwa, muda wa kuweza kurekebisha kasoro na wanaokusikiliza kufanyia hoja zako kwa usahihi.
4: Je ni kweli kuwa hakuna watu wengine kwenye utumishi mpaka sasa wenye matatizo kama hayo au zaidi na bado wanakula mishahara?
5: Je hawa watu hawakuwa na ufanisi wowote pamoja na makandokando yao?
6: Wangapi hawana kandokando kama Mwenyezi Mungu akiamua atumulike wote kwa njia tylizopita? Udanganyifu kwenye mitihani? Udanganyifu kwenye research zetu, kutokutimiza wajibu kwenye kazi?
7: .......
NB: Wakati mwingine tuheshimu busara kama hakuna anaeumizwa moja kwa moja. Kwani hela zilizo kwenye mifuko hiyo ni haki yao, walikatwa wao. Hazitoki kwa mtu mwingine, wapewe wajichange kimaisha kupunguza wategemezi na watu kujinyonga na shida za afya za akili.
Ningeshauri tu wapewe mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupewa hizo hela.