Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Umesikiliza vizuri hotuba yake?
 

Kuna mambi mengi yanayoweza kusababisha mtu kuamua kutumia busara badala ya sheria:

1: Historia ya elimu yetu hapo zamani ilitoa mwanya wa mtu kurudia shule kwa kutumia jina la mtu mwingine, japo si kisheria. Msingi wa majina kutofanana, kwa kutumia hii huko serikalini ni mafuriko hasa wasomi wa siku nyingi.

2: Kutokuwa makini wakati tunajiandikisha kwenye tasisi tofauti kwa kuwa watu hawakujua kama haya yatakuja kutokea.

3: Zoezi lilivyoendeshwa, muda wa kuweza kurekebisha kasoro na wanaokusikiliza kufanyia hoja zako kwa usahihi.

4: Je ni kweli kuwa hakuna watu wengine kwenye utumishi mpaka sasa wenye matatizo kama hayo au zaidi na bado wanakula mishahara?

5: Je hawa watu hawakuwa na ufanisi wowote pamoja na makandokando yao?

6: Wangapi hawana kandokando kama Mwenyezi Mungu akiamua atumulike wote kwa njia tylizopita? Udanganyifu kwenye mitihani? Udanganyifu kwenye research zetu, kutokutimiza wajibu kwenye kazi?

7: .......

NB: Wakati mwingine tuheshimu busara kama hakuna anaeumizwa moja kwa moja. Kwani hela zilizo kwenye mifuko hiyo ni haki yao, walikatwa wao. Hazitoki kwa mtu mwingine, wapewe wajichange kimaisha kupunguza wategemezi na watu kujinyonga na shida za afya za akili.

Ningeshauri tu wapewe mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupewa hizo hela.
 
Hv alisema na wa vyeti feki si Wale wa darasa la Saba tu!!??
 
Mbona wamepokea michango yao kama ni feki.Acha chuki za mwendazake
 
Wewe unahangaika bure mama kaishasema walipwe sikiliza hotuba dakika ya kumi na tatu mpaka kumi na sita , mambo ya roho mbaya za Jiwe hakuna tena .
Ikiwa unaanini watalipwa kweli basi ujue uwezo wako wa kufikilia uko chini sana. Angetaka walipwe wangelipwa akiwa makamu wa rais. Kwa kifupi angetaka walipwe wangekuwa washalipwa.
 
Maoni yako hayana ubinadamu wa kujua hawa watumishi walitumikia hii nchi kuliko hata Jiwe , Wana familia zao na mchango wait wa taifa upo na wamechangia mifuko ya hifadhi ya jamii .
Kwani wewe unacho kipimo cha kujua maoni yepi yana ubinadamu na yepi hayana! Hicho kipimo umekitoa wapi? Kimehalalishwa na nani? Wewe toa maoni yako kisha acha na wengine watoe ya kwao. Hiyo ndiyo demokrasia, siyo?
 
Kwa mantiki kwamba mchakato wa kuwalipa ulikuwa unafanyika sio tamgia uko nyuma sio?
 
Ikiwa unaanini watalipwa kweli basi ujue uwezo wako wa kufikilia uko chini sana. Angetaka walipwe wangelipwa akiwa makamu wa rais. Kwa kifupi angetaka walipwe wangekuwa washalipwa.

Mwingine alitaka kubomoa jengo akazuiwa, alipokuwa baba mwenye nyumba akabomoa.

Kwani wewe unasemaje?
 
Akishafunga watu zaidi 1000 ww utapata amani....
Sio yeye atakayefunga watu 1000 wala mimi kupata kitu chochote,hiyo ni sheria kufuata mkondo mkuu,wapewe haki yao ya mafao ila tusiishie hapo kama walighushi na sheria ina maelekezo yake kwa mtu aliyeghushi,nao ufuatwe halikadhalika.
 
Kwani wewe ni kati ya hao wa vyeti fake mkuu??
Hapana. Nilikuwepo wakati maamuzi yanafikiwa na yalikuwa sahihi kabisa, ila ni sawa tu wakipewa mafao yao maana serikali ilikubali huduma zao hata kama makaratasi ya vyeti yalikuwa ya kilaghai. Kama kuna uwezekano wa kupewa makato yao wapewe. Hakuna tatizo katika hilo.
 
Hili la wa la saba sawa ila hili la vyeti feki hao ni wezi la sivyo walipwe fidia wote waliobomolewa na kukiukwa kwa haki zao
 
Bora eewe umeliona hilo. Akiwalipa vyeti feki atakuwa na tatizo.yaan jitu ligushi vyeti afu alipwe fidia?

Watanzania wanashabekia ujinga.baada ta kupambana vijana wapate kazi wanapambana vyeti feki walipwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…