🤣🤣 Ok. Umejibu ukasahau kuwa hata ardhi yote ni ya serikali, fedha zote n.k ss kwann tuna mihimili mingine?
Serikali haina namna ya kuchukua hizo fedha bila ubabe na kuvunja sheria.
Wenye mamlaka ya kutoa hukumu si serikali ni mahakama, serikali nguvu na mamlaka yake ni kufukuza kazi na kuwashtaki kudai fidia na mahakama ikiona kuna uhalali itatoa hiyo hukumu. Na hukumu inaweza kuwa kifungo, faini au vyote viwili pia inaweza ikatoa maamuzi tofauti ikijiridhisha kuwa wakati unaajiri ulielewa kuwa huyu cheti si halali.
Hakuna njia halali ya kisheria serikali inaweza kuitumia kukwapua hizo pesa kwenye account za mifuko ya jamii bila mahakama.