Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Kwa serikali ya awamu ya 5 hata kama walioondolewa wangepeleka kesi mahakamani hakuna haki ambayo ingetendeka kwa kuwa tunafahamu namna mahakama ilivyofichwa wakati huo.
 
Kitendo cha wenye vyeti feki kuajiriwa kiliwanyima haki wenye vyeti halisi wakakaa bila ajira na familia zao kuteseka kisa mwanga mwenye cheti feki kakalia nafasi zao

Pia kitendo cha cheti feki kuajiriwa kiliwanyima haki wananchi kupata huduma stahiki kutoka kwenye mwenye cheti original wakapewa na mwenye feki
Sawa ila utaratibu wa mashtaka na hukumu kwa hawa matapeli ni upi? Anayetoa hukumu ni nani? Anayeamua kiwango cha hukumu ni nani? Tufate sheria sasa.
 
Uhalali wa kutokupewa mafao ulitakiwa kufata utaratibu upi? Twende taratibu bila mihemko, tujadili tu kwa hoja.
Mwajiri akikuona ulimtapeli anakufukuza kazi na hakulipi, ukiona umeonewa wahi mahakamani wewe.
Serikali ikadaka wenye vyeti feki ikatimua sasa anayeona kaonewa awahi mahakamani
 
Sasa kwanini serikali iliyowaondoa vyeti feki haikuwapeleka mahakamani kama ni jinai? Hujui kuna watu waliondolewa kazini kwa visasi kisa vyeti feki?
Waende mahakamani kuthibitisha hilo wao wa vyeti feki
 
Kazi aliyofanya ni feki

Kazi inatangazwa kuendana na elimu

Mfano inatangazwa kabisa kuwa kazi ya ualimu inataka mtu awe na cheti cha form four na diploma mfano

Wewe huna vyote cha form four huna na cha diploma huna.Unaenda internet cafe kuchonga cheti feki

Wewe DARASA la saba sifa zote huna una ualimu gani uliokuwa ukifanya hapo zaidi ya utapeli kufundisha kiubabaishaji babaishaji tu maana elimu huna.Ukatapeli hadi wazazi wanakuita mwalimu mwalimu wakati ni tapeli tu la mtaani

Mishahara yote uliyolipwa ni pato la utapeli na pensheni uliyopeleka ni sehemu ya mshahara wa utapeli uliotapeli sababu hukutoa mfukoni mwako kupeleka hayo makato yalitoka kwenye mshahara uliotapeli serikali

Hivyo hiyo pension ni mali ya serikali sio yako rudisha na pesa zingine zote ulizolipwa tapeli
Waliofundisha wazazi wako walikua waalimu wa UPE, sema huwezi kuelewa! Jambo la msingi mh. Rais SSH, ameshaamua kwenda kinyume na Mwendazake, Una la kufanya zaidi ya kulialia!?
 
Kwa serikali ya awamu ya 5 hata kama walioondolewa wangepeleka kesi mahakamani hakuna haki ambayo ingetendeka kwa kuwa tunafahamu namna mahakama ilivyofichwa wakati huo.
Serikali ilipaswa kuwashtaki kwa udanganyifu na kufoji vyeti ila stahiki zao wapewe. Kuwaondoa hawa si kwa sababu serikali haikuwajua kabla ni kwa sababu nyingine kabisa, ila waliwajua na hawakuwa na tatizo nao kabla ya sababu iliyojitokeza awamu ya 5.
 
Mwajiri akikuona ulimtapeli anakufukuza kazi na hakulipi ukiona umeonewa wahi mahakamani wewe
Serikali ikadaka wenye vyeti feki ikatimua sasa anayeona kaonewa awahi mahakamani
Sawa, haya mtuhumiwa hajaenda mahakamani kakubali yaishe, serikali nayo haijamshtaki, sasa unajua kuwa zile stahiki tayari serikali ilishamlipa mtuhumiwa, Sema zipo kwenye mifuko ya jamii. Serikali itatumia sheria ipi kuzichukua hizo fedha kwenye account za hawa unaowaita matapeli bila hukumu ya mahakama na bila kuvunja sheria? Maana si pesa zao tena walishafanya malipo.... Tufate tu sheria.
 
Wende mahakamani kuthibitisha hilo wao wa vyeti feki
Jamhuri ndio inapaswa kupeleka na kusimamia kesi za jinai zote mahakamani. Kwa awamu ile ya 5 nani angeenda mahakamani kwani haogopi kupotezwa?
 
Waliofundisha wazazi wako walikua waalimu wa UPE, sema huwezi kuelewa! Jambo la msingi mh. Rais SSH, ameshaamua kwenda kinyume na Mwendazake, Una la kufanya zaidi ya kulialia!?
Sina shida nao walikuwa darasa la saba wenye vyeti halali kabisa vya darasa la saba hao sina shida nao na hadi sasa bado wako wengi tu wanafundisha darasa la kwanza na la pili wengi watu wazima na serikali wala haikuwasumbua na haijawahi wasumbua kama ni hao aligusia kwenye hotuba kama wako ambao hawajalipwa walipwe

Naongelea mitapeli migushi vyeti feki sio hao wa UPE

Ninachopinga kwa nguvu zote ni vyeti feki kulipwa sio sahihi na sidhani ndicho alimaanisha sidhani haipo hiyo lakini kama ni la saba wa UPE wala haina shida na serikali haina shida nao

Hao wenye vyeti feki ndipo maneno yalipo
 
Sawa, haya mtuhumiwa hajaenda mahakamani kakubali yaishe, serikali nayo haijamshtaki, sasa unajua kuwa zile stahiki tayari serikali ilishamlipa mtuhumiwa, Sema zipo kwenye mifuko ya jamii. Serikali itatumia sheria ipi kuzichukua hizo fedha kwenye account za hawa matapeli bila hukumu ya mahakama? Tufate tu sheria.
Hiyo ni juu ya serikali yenyewe sababu ni za kwake kama zilivyo faini za mahakamani inazichukuaje hilo si kazi yangu na yako ni yao wenyewe serikali wenye pesa zao.Watajua wenyewe cha msingi wajue ziko pesa zao
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Hili swala lina mkanganyiko, wako ambao walisoma kwa kutumia majina yasiyo yao wakafaulu, wakaajiliwa hawa wana sifa zote za kitaaluma. Watu wa aina hii huwezi kusema ana cheti feki wakati alivuja jasho! Kwa maoni yangu, hawa walisitahili kustaafishwa na kulipwa stahili zao.
 
Hiyo ni juu ya serikali yenyewe sababu ni za kwake kama zilivyo faini za mahakamani inazichukuaje hilo si kazi yangu na yako ni yao wenyewe serikali wenye pesa zao.Watajua wenyewe cha msingi wajue ziko pesa zao
🤣🤣 Ok. Umejibu ukasahau kuwa hata ardhi yote ni ya serikali, fedha zote n.k ss kwann tuna mihimili mingine?

Serikali haina namna ya kuchukua hizo fedha bila ubabe na kuvunja sheria.
Wenye mamlaka ya kutoa hukumu si serikali ni mahakama, serikali nguvu na mamlaka yake ni kufukuza kazi na kuwashtaki kudai fidia na mahakama ikiona kuna uhalali itatoa hiyo hukumu. Na hukumu inaweza kuwa kifungo, faini au vyote viwili pia inaweza ikatoa maamuzi tofauti ikijiridhisha kuwa wakati unaajiri ulielewa kuwa huyu cheti si halali.
Hakuna njia halali ya kisheria serikali inaweza kuitumia kukwapua hizo pesa kwenye account za mifuko ya jamii bila mahakama.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela.....
Anayetakiwa kuwa jela ni aliyeghushi au aliyeshindwa kuhakiki na kugundua ile fake?

Wengine “walighushi” vyeti vya form four ila wakasomea na wakufuzu vizuri sana taaluma zao kama ualimu, nursing, uhasibu na hawa wamefanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa miaka 20+. Hawa wanaingia fungu lipi?

Hawa watu wamechangia mifuko ya jamii kwa jasho na damu. Hauwezi kuwadhulumu kwa kuwa eti waliforge vyeti vya form iv/vi. Dhambi hailipwi kwa dhambi

Harafu kwanini zoezi lilikuwa la upendeleo mtupu na kuziacha kada nyingine?
 
🤣🤣 Ok. Umejibu ukasahau kuwa hata ardhi yote ni ya serikali, fedha zote n.k ss kwann tuna mihimili mingine?

Serikali haina namna ya kuchukua hizo fedha bila ubabe na kuvunja sheria.
Wenye mamlaka ya kutoa hukumu si serikali ni mahakama, serikali nguvu na mamlaka yake ni kufukuza kazi na kuwashtaki kudai fidia na mahakama ikiona kuna uhalali itatoa hiyo hukumu. Na hukumu inaweza kuwa kifungo, faini au vyote viwili pia inaweza ikatoa maamuzi tofauti ikijiridhisha kuwa wakati unaajiri ulielewa kuwa huyu cheti si halali.
Hakuna njia halali ya kisheria serikali inaweza kuitumia kukwapua hizo pesa kwenye account za mifuko ya jamii bila mahakama.
Asiyeridhika ndie aende mahakamani. Short and clear. Mwenye cheti cha kugushi anayeona alionewa aende mahakamani. Hilo zoezi liliwadaka vyeti feki kwa wingi kuanzia kipindi cha Kikwete na kuhitimishwa kipindi cha Magufuli

Wasioridhika wenye vyeti feki waende MAHAKAMANI
 
Sina shida nao walikuwa darasa la saba wenye vyeti halali kabisa vya darasa la saba hao sina shida nao na hadi sasa bado wako wengi tu wanafundisha darasa la kwanza na la pili wengi watu wazima na serikali wala haikuwasumbua na haijawahi wasumbua kama ni hao aligusia kwenye hotuba kama wako ambao hawajalipwa walipwe

Naongelea mitapeli migushi vyeti feki sio hao wa UPE

Ninachopinga kwa nguvu zote ni vyeti feki kulipwa sio sahihi na sidhani ndicho alimaanisha sidhani haipo hiyo lakini kama ni la saba wa UPE wala haina shida na serikali haina shida nao
Sababu ya vyeti feki na kila aina ya kufoji ni mfumo mbovu wa utawala chini ya CCM kwa miaka 60!
Wapo wenye vyeti feki ambao walifanya kazi nzuri, za udaktari, ualimu na zinginezo, kuliko hata hao wenye vyeti ‘halali’!
Pia, utumbuaji ulikua wa kukurupuka, kama ni hao watu 10 wanatumia jina moja kufanya kazi hiyo hiyo ni wizi, lakini kuna ambao walisoma kwa majina yasiyo kuwa yao, lakini ni wajuzi! Kwa mfano, hapa kuna Mtu katoa mfano hapa wa dereva aliye fanya kazi kwa miaka 30! Hana cheti cha form 4 kama sheria inavyo taka, leo unamtumbua kisa cheti?! Kwani cheti ndo kiliendesha gari?!

Pia kuna wenye vyeti kabisa, lakini wamehonga ufaulu wao tangu darasa la 7, alafu sasa ni watu wazito serikalini, unasemaje hao?!
 
, hapa kuna Mtu katoa mfano hapa wa dereva aliye fanya kazi kwa miaka 30! Hana cheti cha form 4 kama sheria inavyo taka, leo unamtumbua kisa cheti?! Kwani cheti ndo kiliendesha gari?!
Hapo ndipo mnapoonyesha ujinga mliona. Hapo hakuna dereva, kazi inataka mtu awe kamaliza form four na cheti cha ufundi magari cha Veta, yeye hana anafoji. Gari za serikali ndio maana nyingi tu ulikuwa unazikuta ziko kwenye mawe wakati zinaonekana ni kama mpya sababu mwendeshaji hana ujuzi wowote wa utunzaji gari wala kujua hata lina tatizo lipi, anajua tu kupeleka gari mbele na kurudisha reverse!!! Mpaka linafikia ubovu wa kufa kabisa
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Wa vyeti feki hawajatajwa mkuu usipaniki, watakaolipwa ni wale wenye elimu ya darasa la saba au wasio na vyeti vya form four
 
Hiyo ni juu ya serikali yenyewe sababu ni za kwake kama zilivyo faini za mahakamani inazichukuaje hilo si kazi yangu na yako ni yao wenyewe serikali wenye pesa zao.Watajua wenyewe cha msingi wajue ziko pesa zao
Kuna tatizo kidogo kuhusu imani yako kuhusu serikali na pesa za serikali, kupitia mtazamo wako huu!
Kwa taarifa yako, serikali ni ya wananchi na pesa zote, ni mali yetu wananchi, not more nor less!
 
Back
Top Bottom