Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
1725809585024.png

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
 
Imani ishashuka na wananchi wanaanza kuisusa serikali kwasababu kwakauli yake rais alisema hizi ni drama na spika akasema hakuna la kuongelea juu ya utekaji maana haya mambo hayapo Mungu atunusuru watu wasiichoke serikali wakaanza kujilinda binafsi na kulipa kisasi sawia.
 
Anatekwa hakujitokeza kuagiza uchunguzi.

Mama unatuangusha sana, mimi ni miongopi tuliokuunga mkono mwanzoni. Ila this is too much asee. Inawezekana haya matukio yasiwe na baraka zako lakini kwa nafasi yako unaweza kuyakomesha.

Kuna yatima wapya na mjane mpya mtaani. Mungu na asimame upande wa walio wema.
 
Back
Top Bottom