Ninaamini kauli hii ya Rais Samia ni ya dhati. Ukweli ni kwamba ndugu yetu Ally ametekwa na kuuawa na kile kinachojiita kikosi kazi/task force. Ndani yake wamo polisi, TISS na JWTZ. Sasa vyombo alivyoviagiza Rais vifanye uchunguzi, ni chombo gani nje ya hawa wahusika wakuu?
Hiki kikosi cha kiharamia kisipovunjwa na kupotezwa, kadiri kinavyozidi kunogewa na damu za watu, kuna siku kinaweza kuwageukia hata wao wenyewe au wapendwa wao.
Hawa wauaji, Rais Samia amewalea mwenyewe. Watu wanatekwa na kuuawa, yeye anasema kuwa eti ni drama!! Halafu akaongeza kwa kusema kuwa eti anawapongeza nchi imekuwa shwari. Baada ya hizo pongezi, wakaongeza uovu.