Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Jibu mwenyewe utakavyo
Nakubali , kwanza pia hii inahusu Magari ya police yote yabadilishwe rangi , au yawe na code inayotambulika kwa raia , mfano leo nikiwa dar najua nimepanda daladala ya kwenda posta, ubungo ,mbagala , mbezi ,gongo la mboto, n.k

Magari ya police yawe na code , nje ya iyo code basi wanakuja ni vibaka wakabiriwe kadri walivyokuja .

Hii naunga mkono
 
Polisi wakikukamata si unapelekwa kwenye vyombo vya sheria? Hawa wengine ambao hawajulikani wako wapi, nani amewachukua?
Ni hatari sana. Wahuni wanaweza kumpora tajiri, wafanyabiashara mpinzani wao kibiashara, kisiasa, kifamilia. Wakavaa jezi za polisi na magari yao navitambulisho feki nani anawasimamisha?.
 
So what, ndo hivyo mzee hatunae tena ,ingekua ni deni ,lingelipwa , ingekua ni kifungo bado ndugu na jamaa wangekua na matumain kwamba ipo suku kitaisha , sasa uhai hauna mbadala , dadekii nimeumia sana ,sana ,sana sana
Naomba kuuliza, hivi huyu marehemu alikua anafanya biashara gani!? Isije kua hii ni vita ya kiuchumi ya Kimyakimya!!
 
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
Imeisha hyoo..
 
Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
 
Kwakuwa inadaiwa marehemu alikamatwa na watu wenye silaha basi kabla ya hiyo ripoti ni muhimu sana Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akajiuzulu pamoja na IGP. Ofisi za umma ni kwaajili ya kuutumikia umma, na hiyo kazi wao imewashinda!

Kama hao watu ni Polisi, basi tatizo ni kubwa, na kama sio polisi basi tatizo ni kubwa zaidi.
 
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
Bivi una weza kumuaviza mwizi akuletee taarifa za wizi?
Wananchi wa kada mbalimbali wameomba uunde tume kuchunguza haya. Mauaji na kuteka ume kaa kimya ati leo akuletee taarifa!! Lini!!! Hii ni janja ya nyani kula mahindi mbichi.. Hatuoni uhalali wa hili agizo zaidi ya kuendelea kuona kama Drama
Tuli tegemea kusikia ume muodoa IGP na Waziri wake, hata Simba Chawene na mkurugenzi wa TISS. Lakini una tufumba macho hapa.
Lakini iko siku yaja tusiyo ijua haya machozi ya Watanzania yatakuwa maji ya zabibu. Mungu hachelewi kwa wamuombao
 
Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
Sidhani kama kulikuwa na kesi iliyosimama dhidi ya mbowe. Mbowe ni mfanyabiashara hawezi kufanya ugaidi. Ni tabaka la utawala Tanzania. Wote wakuu wa nchi ni marafiki wake.
 
Sasa huyu kawaida, hapa amereason, ameona ni jambo la maana akaamua kuandika Twitter kabisa? Ninyi UVCCM akili zipo kweli? Reasoning gani hii ya mtu mzima?

Yawezekana mimi nilikuwa najua kuwa fulani ametekwa najua wa kwanza nikaamua kutokutoa taarifa public, ila nikampa taarifa mtu ambaye akaipeleka Public, Na hivyo hivyo taarifa ya kupatikana Mwili wasamaria/staged wamepiga simu polisi, ila polisi hawajatoa taarifa public, alivyoipata Boniface akaipeleka public wa kwanza, ajabu nini sasa kwa mtu kutoa taarifa za kutekwa na kupatikana mwili wa kwanza, ikiwa kuna wengine wamepata taarifa na kuamua kukaa kimya?

UVCCM nawaonea huruma sana , kwa kipi mnacholipwa mnajitoa ufahamu hivi? mishahara yenu yenyewe hiyo kama ya Polisi ndio inawatoa utu hivi? Au hizo posho mbuzi za hapa na pale? Mtu unakubali kutumika kama toilet paper namna hii hata kesho yako huijui!? 🚮
 
Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.
Hata Magufuli alisema vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze nani wamehusika kumpiga risasi Lissu
 
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
Kwa hili kura yangu naipeleka chauma
 
Back
Top Bottom