Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Vyombo vya ulinzi na usalama ni washukiwa vipi wajichunguze!??
 
Tayari wewe ni kati ya lile kundi la wenye akili ndogo
 
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu ameshaagiza. Tuvipe nafasi vyombo vya usalama.

Kikubwa naomba tujadili tukiwa Watanzania wazalendo: 1. Tukisingizia polisi kila tukio ipo siku magenge ya kihalifu yatatumia mwanya huo kutekeleza uovu.

Kwa mfano, leo hii genge la wahalifu hata la nje ya nchi linaweza mnyakua Mbowe au Lissu wakijua watalaumiwa polisi. Tulishuhudia dada yule kutoka ukoo wa Jaji Kamana, alitekwa na kukatwa katwa viungo na mpenzi wake, watu wanapotea kumbe wengine wamezikwa kwa Mganga Singida. Point yangu ni ipi? Kila raia ajue usalama wake unaanzia kwake, tusinyooshee kidole sana Jeshi la Polisi bali tuungane kulisaidia. Pili, tuchambue nature ya matukio. Haiti, Colombia na Ecuador kuna magenge ya kihalifu yanalenga kuzikosesha serikali na wananchi utulivu. Tuungane kujenga umoja wetu na kuilinda amani yetu.🙏🙏🙏
 
Wanashutumu, bila ushahidi wa maana, idara Yako nyeti inayotutulizia nchi hii.

Wanakushutumu waziwazi wewe na matusi juu. Bila nukta yoyote ya ushahidi.

Wanatengeneza Kila mazingira ya kulihusisha jeshi letu la polisi Ili kulipotezea heshima na kutafuta umaarufu.

Kauli zako Mama, za kukemea haya mauaji, nashauri zitoe kwa uangalifu wa Hali ya juu mno.....ukikosea kidogo tu umeingia kwenye kumi na nane zao. Kikwete alihangaika sana na hili, ni JPM tu angalau aliwajulia.

Nawasilisha.

nb:
Leo msibani tayari wameshaanza kulishutumu jeshi la polisi.
Comments reserved
 
🚽
Takataka halafu na wewe ndio unamshauri rais, hivi akili zenu huwa zinakuwa na tatizo gani? Hivi haya matukio ya mauaji yanayotokea kila siku wewe unayachukuliaje?
 
Amelipwa kwa kifo cha kikatili inasikitisha mno
Yaani viongozi wachadema kwa sasa wanawinda kama viongozi wa Hamas. Wanapaswa wajiadhali sana hasa wa mikoa kama, mbeya, mwanza,arusha. kilimanjaro, arusha yaani mikoa yote ambayo upinzani umeshamiri sana. Jili wimbi litaendelea mpaka uchaguzi wa Rais na madiwani upite kisha viongozi watakaa kutafuta muafaka.
 
Back
Top Bottom