Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao


Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
Kwakweli hili tukio limeniumiza sana nikiwaza familia yake watoto wake na watu waliokuwa wakimtegemea ,huyu mzee simfahamu ila kwa muonekano wa haraka ni muungwana ila mungu wa haki yupo na huwa hapangiwi ,hachelewi wal awahi, tumuachie yeye anayeona tusiyoyaona na anayajua tusiyoyajua
 
Watanzania hawabebeki, wamekaa pembeni hawawezi kuandamana kupinga kuonewa, kunyanyaswa, kupuuzwa, kutekwa na kuonewa


View: https://m.youtube.com/watch?v=j6gscHNQl-c
Polisi watumika na utawala wa CCM ku testi hulka ya watanzania kama wanaweza kukasirika na kuandamana kuondoa utawala uliopo madarakani kwa kufanya yafuatayo :
  • 2024 Mzee Ally Mohamed Kibao atekwa akiwa ndani ya basi la TASHRIF na kuuawa
  • 2024 Wanachama 500 wa CHADEMA wakamatwa nchi nzima 11 Agosti 2024 kuelekea siku ya Vijana Duniani Mbeya
  • 2024 Vijana Deus Soka, Kombo Mbwana, Sativa wakamatwa bila kufikishwa mahakamani
  • 2024 Tundu Lissu anatoa elimu ya Uraia lakini watanzania ni waoga
  • Serikali inatayarisha uchaguzi wa TAMISEMI November 2024
  • Ardhi za wananchi kule nyika za Ngorongoro na kule Mbozi kwenye kimondo wananchi wapo kimya
  • 2017 mheshimiwa Tundu Lissu apigwa risasi mjini Dodoma
  • 2021 mheshimiwa Freeman Mbowe atiwa mbaroni mjini Mwanza na kufunguliwa kesi ya ugaidi
  • 2019 viongozi wote wa vyama mbadala wa vijijini, vitongoji na mitaa waenguliwa
  • 2020 uchaguzi mzima waporwa, wananchi wapo kimya
  • Bunge, Mahakama na dola zimetekwa nyara (state capture)na taasisi ya urais
  • Watanzania wamekuwa mateka katika gereza la wazi nchi nzima ya Tanzania
  • N.k
Mazito kwa kina Utekaji wa Kimkakati : Vikosi maalum vya Task Force vilivyo nje ya mfumo rasmi, na vikosi hivyo kupewa mamlaka kupitia sheria iliyotungwa na bunge inayoruhusu member wa task force kuua bila kufikishwa mbele ya vyombo vya haki yaani mahakama

Mateso ya kimyakimya : Sheikh Ponda azungumzia kifo cha Ali Mohamed Kibao


View: https://m.youtube.com/watch?v=rNfxIHqdzME
 
1:Waziri wa Mambo ya Ndani bado Yuko Ofisini?
2:IGP bado yupo Ofisini?
Sisemi wanahusika, Kwa Mazingira na Hali ilivyo hata Kwa Kujihudhuru wenyewe ili kulinda heshima zao pia konesha kutokunaliana na Hali.
Rais wachukulie hatua kama sehemu ya uwajibikaji, Serikali inapakwa Matope na watu wachache,hatujazoea kuyaona haya.
Kizazi kitageuka na kubadili tabia tutakuwa Afughastani,watu wanajitoa mhanga Kila mahali.
Emungu epusha hili,Rais epusha hili.
Narudia hatujazoea kuyaona haya.
 
Kinafiki tu. Siku akipata hadhara ya kuhutubia ataanza kuongea vijembe vyake kuwa ni drama.

Siku atayo address hili swala kwa dhati ni siku wahalifu wake wakimuumizia kizazi chake na yeye.
Ofcourse ni kinafiki. Kuliko angekaa kimya. kuna normies wakiona raisi ameli-adress suala kama hili, wanajua serikali haihusiki
 
Ninaamini kauli hii ya Rais Samia ni ya dhati. Ukweli ni kwamba ndugu yetu Ally ametekwa na kuuawa na kile kinachojiita kikosi kazi/task force. Ndani yake wamo polisi, TISS na JWTZ. Sasa vyombo alivyoviagiza Rais vifanye uchunguzi, ni chombo gani nje ya hawa wahusika wakuu?

Hiki kikosi cha kiharamia kisipovunjwa na kupotezwa, kadiri kinavyozidi kunogewa na damu za watu, kuna siku kinaweza kuwageukia hata wao wenyewe au wapendwa wao.

Hawa wauaji, Rais Samia amewalea mwenyewe. Watu wanatekwa na kuuawa, yeye anasema kuwa eti ni drama!! Halafu akaongeza kwa kusema kuwa eti anawapongeza nchi imekuwa shwari. Baada ya hizo pongezi, wakaongeza uovu.
 
Binafsi sitaki serikali ya Tanzania ichunguze kifo hiki na Nachukua Nafasi hii kuwakataza kabisa Viongozi wa Chadema kukubaliana na hili
si muhimu,
Lakini uchunguzi ni Lazima utafanyika kwa mujibu wa sheria na kulingana na maagizo ya Mkuu wa nchi, hakuna hiyari kwenye hili 🐒
 

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.

Pia Soma:
At least amejitokeza. Kimya kilikua kinaibua maswali mazito sana
 
Back
Top Bottom