Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Bila kusahau hasara waliyoisababisha kwa kutoa huduma hafifu kutokana na kutokuwa na maarifa yanayotakiwa
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Hajatoa maagizo ya moja kwa moja. Bali amesema ipigwe hesabu kuona itagharimu kiasi gani kwa waliobakiza mwaka mmoja au miwili walipwe. Ila mpaka hesabu zipivwe waone kama wanaweza kuwalipa
 
Ameagiza walipwe 5% walizokatwa. Zile 5% na kwa wale waliobakiza mwaka mmoja kustaafu serikali itakaa iangalie gharama ione itafanya nini.
 
Kama ni haki yao basi walipwe tu.
Hata waliodhulumiwa ushindi wao kwenye uchaguzi 2020 walipwe haki zao ikiwemo kupewa ushindi waliodhulumiwa.
Hata Tundu Lissu alipwe haki zake zote za matibabu na kuvuliwa ubunge wake kihuni.

Kama kuna mtu kanyang'anywa haki zake pasipo halali ni vyema akarudishiwa haki zake. Kila mtu apewe haki zake.

Na kama kuna mtu aliiba haki za mtu mwingine au alilipwa haki isiyostahili ni vyema haki hiyo akanyang'anywa na akalazimishwa kuiresha kule alikoiiba. Mfano ni wale wabunge wa Covid 19. Wale ni wezi na malaya walioiba haki za kisiasa, wachukuliwe hatua mara moja.
 
Hajatoa maagizo ya moja kwa moja. Bali amesema ipigwe hesabu kuona itagharimu kiasi gani kwa waliobakiza mwaka mmoja au miwili walipwe. Ila mpaka hesabu zipivwe waone kama wanaweza kuwalipa
Sasa si ndio mchakato wa kuwalipa huo?
 
Hajatoa maagizo ya moja kwa moja. Bali amesema ipigwe hesabu kuona itagharimu kiasi gani kwa waliobakiza mwaka mmoja au miwili walipwe. Ila mpaka hesabu zipivwe waone kama wanaweza kuwalipa
Wengine wote watalipwa 5% ya salary waliokatwa.....kwenda mifuko jamii...wataambulia kitu
 
Back
Top Bottom