Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Hii nchi nzuri sana.

Unaiba halafu unalipwa.

Hongereni kwa kulipa wezi.
Hili jambo lisingekuwa na mwisho mzuri kama lingebaki hivi, Katika kuadhibu tunaadhibiana kwa akili ili kurekebishana sio nguvu tu kwa sababu tunazo na tunaweza kuadhibu.

Mtu kakutumikia miaka 30 ukagundua aligushi cheti cha form four, anastahili adhabu ni kweli, lakini sio kwa kukata mikono yake ili asiweze kufanya kazi tena, asiwe sehemu ya uchumi wako tena awe tegemezi 100%.

Kufanya hivyo ni kujipa mzigo maana ni mwananchi wako. Aadhibiwe lakini kwa kutumia ubinadamu na upimaji wa kosa na adhabu anayostahili.

Kuwapa 5% ya makato waliyokatwa wakati wanafanya kazi raisi katumia busara kulizika hili suala rasmi.

Sasa si rahisi usikie malalamiko ya kuomba huruma kutoka kwa watu hawa tena, watumie hicho watakachojipata kuanzisha biashara halali na serikali iwe makini katika kuajiri jambo hili lisijirudie.
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Mkuu; Swali lako hapo mwisho kama likizingatiwa kwa mujibu wa maneno yako ni HATARI kweli-kweli. Kama HAKI itazingatiwa basi ni vizuri waanze na waliowaajiri au tuseme wale walioridhika na Documents zao na kuwaingiza kazini. i.e. Waziri/Katibu mkuu/DED e.tc. wote wawajibishwe kwa pamoja wao na walioingia kazini.
Ni haki yao walipwe makato yao yaliyopelekwa kwenye mifuko ya Jamii, na kwa wale waliotumikia zaidi ya miaka 15 walipwe mafao ya kustaafu- Hii ni kwa Mujibu wa Taratibu za ki-Utumishi Serikalini.
Lakini yote kwa yote Mkuu; Ingefaa uzingatie kwamba ufanyaji / utendaji wa Serikali (sio Tz. tu, bali serikali au Taasisi zingine) mambo yote na maagizo yote ya ki-Serikali ni kwa Maandishi na ni kutoka kwa Mtu au Ofisi yenye Dhamana hiyo. Huku jukwaani tunalumbana tu. Ukiona limetoka Tangazo/Agizo Rasmi ujue ndo imepitishwa. Raisi kuzungumza katika Hotuba (Kama ni kweli) haijawa Agizo. Je, Mh. Raisi wa JMT alisema "Naagiza....."?? Endapo hakusema hivyo, basi Tusubiri kwanza kwani hujapewa hiyo kazi ya kutoa Tangazo.
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Ni haki yao kabisa. Tuache zulma, tuangalie makosa yalikuwa upande gani? Serikali ndiyo iliwaingiza halafu wewe unakuja humu Jf unawatukana. Halafu unakuta huyo huyo ndiye kamnusuru mama yako na wewe ulipozaliewa. Tuambizane ukweli. Hata Mimi lazima wapo walionisaidia mpaka hapa nilipo japo siwajui

Mkosoeni na nyerere kwa Nini aliajiri watu mitaani kwenda kufundisha? Kuwa maaskari n k.

Sheriakuwa zinafa yiwa kazi hawa watu wasimgeingia humo.

Mama walipe tu. Hawa wanaowakejeli waache wafe na vidomda vya matumbo.

Acheni roho mbaya. Kama huna kazi usivizie godoro la mwezio ndiyo ulale. Tafuta la kwako.

Kama serika imeshapata mwarubani nivizuri ili na nyiyi mnaokejeli humu mpate mapesa na ajira.

Acheni kumnyooshea mwenzenu vidole inawezekana alikuwa hajui
Mnajua Sheria nazo ni changamoto. Ile lugha ya kimombo.
 
Kuajiriwa na mamlaka sahihi haiondoi ukweli kwamba walighushi.
Tusitoe adhabu kama mashetani. Tuwe na kipimo cha adhabu. Samia hajakosea kutowarudisha kazini na kuwapa hizo 5% walizokatwa.
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Walipwe
 
Je ! Ni sahihi kutowalipa ilhali walikatwa pesa zao na walilitumikia taifa kwa haki!??
Walitumikia taifa kwa njia isiyo halali kupitia vyeti walivyokuwa navyo ndiyo maana ndiyo maana hadi sasa tuna kizazi cha kusifu na kuabudu kwani waliowengi walitengenezwa na watu hao, bado wapo wengi sana hawajaisha! Unatafta cheti cha shahada unaajiriwa na serikali mtu wa hivo unafikri atakuwa wa aina gani na wakiwa watano sehemu moja unafikri serikali wataisema kwa lolote hata kama kuna baya[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Wanastahili kulipwa kwa kazi waliofanya, hongera Samia.
 
Walitumikia taifa kwa njia isiyo halali kupitia vyeti walivyokuwa navyo ndiyo maana ndiyo maana hadi sasa tuna kizazi cha kusifu na kuabudu kwani waliowengi walitengenezwa na watu hao, bado wapo wengi sana hawajaisha! Unatafta cheti cha shahada unaajiriwa na serikali mtu wa hivo unafikri atakuwa wa aina gani na wakiwa watano sehemu moja unafikri serikali wataisema kwa lolote hata kama kuna baya[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
Acheni wivu... hamna jema nyinyi!??
 
Kwa Haki vipi na cheti FEKI?
Je ungekuwa wewe ungeongea hivi? Je kilichofanya kazi muda wote ni cheti au huyo mtumishi? je unauhakika gani katika ndugu au jamaa zako hakuna aliyepitia haya? maisha ni kuhangaika mtu hajaiba amehangaika kutafuta maisha wewe unakuja na kauli hii.Mama yupo sahihi na Mungu tunaomba amlipe mema.Fikiria kuna waliokutibu hospitali, somesha, kukuhudumia kwa njia yoyote ile.
 
Mamá Samia hakupaswa kabisa sio tu kulitamka bali hata kulifikiria hili swala

Maana hawa wa vyeti feki wana hatia ya kuidanganya Serikali na kupatiwa mishahara isivyo halali

Jpm alikuwa na huruma ila kiutaratibu walitakiwa kufunguliwa mashtaka ya kufoji na kujipatia pesa isivyo halali
 
Back
Top Bottom