Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Nafahamu mazingira yaliyopelekea hivi vyeti feki kuwa vingi namna hii maana wengine tumekuwa tukishuhidia utendaji wao na kuziona kazi zao kwa miaka mingi.

Hawa watu wengi walifoji vyeti waliajiriwa kihalali kabisa ila baada ya kufanya kazi muda mrefu na serikali kutaka wajiendeleze walikubali ila kurudi shule wakakuta si sawa na uzoefu walio nao huku makazini, kama unavyojua elimu yetu ni kukariri formular, magazijuto n.k wakashindwa na wakashawishika kutumia shortcut. HILI LILIKUWA KOSA na lilistahili adhabu ila si ya kiwango cha kuwanyima hata hizo 5% walizokatwa.

Wengine walifeli masomoni kabla ya ajira, wakanunua cheti(HILI LILIKUWA KOSA) halafu wakasoma kihalali mpaka degree na kuendelea, wakaajiriwa. Wanastahili adhabu lakini si ya kiwango cha kuwanyima hata hizo 5% walizokatwa.
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Ni sahihi sababu walitumika kujenga Taifa.Akili zao zilitumika na sio vyeti vyao
 
Nafahamu mazingira yaliyopelekea hivi vyeti feki kuwa vingi namna hii maana wengine tumekuwa tukishuhidia utendaji wao na kuziona kazi zao kwa miaka mingi.

Hawa watu wengi walifoji vyeti waliajiriwa kihalali kabisa ila baada ya kufanya kazi muda mrefu na serikali kutaka wajiendeleze walikubali ila kurudi shule wakakuta si sawa na uzoefu walio nao huku makazini, kama unavyojua elimu yetu ni kukariri formular, magazijuto n.k wakashindwa na wakashawishika kutumia shortcut. HILI LILIKUWA KOSA na lilistahili adhabu ila si ya kiwango cha kuwanyima hata hizo 5% walizokatwa.

Wengine walifeli masomoni kabla ya ajira, wakanunua cheti(HILI LILIKUWA KOSA) halafu wakasoma kihalali mpaka degree na kuendelea, wakaajiriwa. Wanastahili adhabu lakini si ya kiwango cha kuwanyima hata hizo 5% walizokatwa.
Adhabu ipi? Wakifunguliwa mashtaka pia mtakuja kusema wanaonewa? Adhabu ipi inawafaa?
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Cheti Ni tatizo, Lakini dogo! Suala la msingi wamefanya kazi zinazostahili malipo na hatimaye mafao, ambayo kimsingi yamekatwa kwenye mapato yao?! Kwani Ni cheti, kiwe original Au fake, kilicho fanya kazi?
 
Mamá Samia hakupaswa kabisa sio tu kulitamka bali hata kulifikiria hili swala

Maana hawa wa vyeti feki wana hatia ya kuidanganya Serikali na kupatiwa mishahara isivyo halali

Jpm alikuwa na huruma ila kiutaratibu walitakiwa kufunguliwa mashtaka ya kufoji na kujipatia pesa isivyo halali
Sio kwamba alikuwa na huruma, ni kwamba alihitaji kupunguza wafanyakazi bila gharama kubwa na akatumia makosa ya hao watumishi kutimiza takwa lake hilo.

Angewashtaki huenda mahakama ingetenda haki kama ingeachwa huru, Serikali ingepata haki yake na matapeli wangehukumiwa kulingana na makosa waliyotenda.

JPM (RIP) Alitake advantage ya kuwa mwajiri ambaye ni amiri jeshi mkuu na mtumishi yupi angekubali kwenda mahakamani kupambana na JPM?
 
Siwezi kuvaa viatu vya majizi ya kitaaluma.

Mimi nimesoma nimeenda shule bwana. Siwezi kuwa sambamba na majizi ya vyeti.

Tumeelewana? Au niongeze sauti ya redio?
Hao unaowaita majizi wengine walikuhudumia wewe kima ww.
 
Back
Top Bottom