Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Umefoji vyeti. Umetumia laghai kazini na kwenye biashara. Hujafungwa. Bado wataka kulipwa?! Au walipwe?!
Bongo kweli banana republic…
Washitakiwe wale waliotoa ajira !! Haiwezekani umfanyishe MTU kazi miaka mingi baadaye umfukuze kazi na usimlipe stahiki zake !! Ni kwanini hukuvichunguza hivyo vyeti kabla hujawaajiri ??
 
Je ungekuwa wewe ungeongea hivi? Je kilichofanya kazi muda wote ni cheti au huyo mtumishi? je unauhakika gani katika ndugu au jamaa zako hakuna aliyepitia haya? maisha ni kuhangaika mtu hajaiba amehangaika kutafuta maisha wewe unakuja na kauli hii.Mama yupo sahihi na Mungu tunaomba amlipe mema.Fikiria kuna waliokutibu hospitali, somesha, kukuhudumia kwa njia yoyote ile.
Kwanza ni kitu cha ajabu sana kwani cheti ndicho kinachofanya kazi au ni MTU ndiye anayefanya kazi ?? Kama angekuwa haimudu ile kazi huyo MTU asingevumiliwa kazini muda wote huo !!
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Serikali yenyewe hii iko madarakani kwa kutenda uhalifu wakati wa uchaguzi, kwanini wawanyime haki yao wahalifu wenzao? Magu aliyeondoa wenzake kwa vyeti fake yeye mwenyewe alikuwa na PhD fake.
 
Kwa Haki vipi na cheti FEKI?
Nani aliwaingiza hao fake?? serikali iliwahitaji ikapiga kimya kwa awamu zote hizo??? je walijiingiza wao wenyewe bila serikali kuwafanyia tathmini?? hawakuhakikiwa wizara husika kabla??..... hivyo vyeti si viko computerised au mie ndo sielewi!!

Je Baraza la mitihani waliwajibishwa au walijitengenezea ivo vyeti??
 
Ni kama mtu anavyoweza kwenda dukani na hela feki na mwenye duka asimgundue, huwezi kumlaumu victim
Kwanza kabisa, hatujui hata kama tuhuma ni za kweli, hatujui makubaliano ya ajira yalikuwaje.

Mchakato mzima umeendeshwa kibabe sana, watu hawakusikilizwa katika due process.

Kuna watu wamebadilisha majina tu wakaambiwa wana vyeti feki, ni wengi sana hawa.
 
Mamá Samia hakupaswa kabisa sio tu kulitamka bali hata kulifikiria hili swala

Maana hawa wa vyeti feki wana hatia ya kuidanganya Serikali na kupatiwa mishahara isivyo halali

Jpm alikuwa na huruma ila kiutaratibu walitakiwa kufunguliwa mashtaka ya kufoji na kujipatia pesa isivyo halali
Kama alifoji na akaitumikia nchi kwa uaminifu sioni kosa! kwa kuwa alijiendeleza kwa manufaa ya kusaidia watu!! Mataifa makubwa mpaka leo wanaibiana teknolojia! za kila kitu na mwizi unapewa Reward!!

Hizo Nuclear zote ni wizi mtupu!!...rejea '' OPeration Paper clip!!'' hapa waliiiba mafaili mpaka wakaona hayatoshi wakaiba wataalamu kabisa wakawang;oa Ujermani wakawapeleka USA!! .... wizi ule uliwafanya USA kuishinda Ujermani na washirika wake faster!!

USA tangia hapo akawa kidedea!! ...sasa nyie Maskini hamtaki mnawapa majina mabaya eti wezi.... Kaburu linawacheka sana. nchi yenyewe haina wataalamu....Mzungu alikuwa anawarusha madarasa watoto wenye uelewa mkubwa, km kin kambona . Nyerere. tuntemekenk!

Wewe Mmatumbi na Rais wako huyo mfu mnaona ni dhambi!!...wkt Nyerere alilifanya hili wkt nchi haina wataalamu!! leo limekuja hilo linakurupuka hovyo!!! kuumbe lenyewe ndo jizi number moja! Mungu akakata ulinzi! likafa!

Wizi kama huu Nyerere aliuita wizi wa mbolea!!...Mtu akiiba mbolea akapeleka shambani kukuza mazao watu wale ......eti zezeta unamkamata??.....na kumzodoa...... nani mwenye akili hapo???
 
Kisheria si sawa na ilitakiwa wawe ndani wanatumikia vifungo

Lakini kibinadamu ni sawa kabisa..
Nimejaribu kuvaa viatu vyao..Kuna watu walikuwa na wategemezi Kwa hiyohiyo kazi na hayo mafao yalipangiwa bajeti.
 
Nani aliwaingiza hao fake?? serikali iliwahitaji ikapiga kimya kwa awamu zote hizo??? je walijiingiza wao wenyewe bila serikali kuwafanyia tathmini?? hawakuhakikiwa wizara husika kabla??..... hivyo vyeti si viko computerised au mie ndo sielewi!!

Je Baraza la mitihani waliwajibishwa au walijitengenezea ivo vyeti??
Ukipita na madawa ya kulevya uwanja wa ndege ... eti kwa sababu ulikaguliwa ndio hayo madawa yanakua halali?
 
Kwani aliyewaajiri si aliwahakiki kwa vyeti na ufanisi wa kazi na akaridhika nao? Au waliizuia serikali kuhakiki taarifa zao?
Uhakiki hauna mwisho ni kama ukaguzi tu bandarini kuna wanaopitisha meno ya Tembo hapohapo na kuna wanaokamatwa... arobaini yao ilikua awamu ya tano ...Hata hivyo jinai haifi.
 
Back
Top Bottom