Rais Samia aahidi kupandisha mishahara watumishi wa serikali

Rais Samia aahidi kupandisha mishahara watumishi wa serikali

Huko Kenya ni mwaka wa Uchaguzi na kuna msuguano sana.Imebidi Rais Kenyatta aongeze mishahara mwezi Mei ili kupunguza nguvu za Kambi ya Ruto kwenye uchaguzi wa Augusti mwaka huu.

Uchaguzi wa 2020 mbona dhalimu hakupandisha hapa?
 
KWA maono yako hayo utakuwa mwalimu au mgambo maisha yamepanda hivi unawaza elfu 50
Ha ha ha ha

Whatever

Mwalimu analipwa mshahara mzuri tu kulingana na elimu yake

By ze way walimu ni watu wa muhimu sana kwa maisha yako,usingeweza kuingia JF bila mwalimu, waheshimu.

Mgambo?? Sijui kama wapo kwenye utumishi wa umma
 
01 May 2022
Nairobi, Kenya


Mshahara wa chini kabisa sekta ya umma waongezwa kwa asilimia 12


Mshahara Wa Chini Kabisa Sekta Ya Umma Waongezwa Kwa Asilimia 12​

NA SAMMY WAWERU

SERIKALI imetangaza Jumapili nyongeza ya asilimia 12 kwa wanaolipwa mshahara wa chini kabisa katika sekta ya umma.


Tangazo hilo limetolewa na Rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Nyayo, Nairobi wakati wa sherehe za Leba Dei, Mei 1, 2022.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta amesema serikali yake inaelewa changamoto ambazo wafanyakazi wanapitia hususan kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

“Hayo yanatushawishi kutathmini kiwango cha mshahara wa chini kwa nyongeza ya asilimia 12, kuanzia Mei 1, 2022, yaani leo,” kiongozi wa nchi akatangaza.

Mabadiliko hayo ya malipo hata hivyo yatatekelezwa kwa wafanyakazi walio katika sekta ya umma pekee, walioajiriwa na serikali.

Nyongeza hiyo inaashiria, mfano, anayelipwa mshahara wa Sh50, 000 kwa mwezi, atapata nyongeza ya Sh6, 000.

Hii ina maana kuwa atapata jumla ya Sh56, 000, kabla kuondolewa kwa ushuru wa PAYE, malipo ya mafao ya uzeeni (NSSF), bima ya afya (NHIF) na makato mengine ya serikali.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini (Cotu) ni Francis Atwoli.

Tangu janga la corona lilipotua nchini Machi 2020, gharama ya maisha imeendelea kupanda, bidhaa muhimu za kimsingi kama vile vyakula vikiandikisha mfumko wa bei.

Mafuta ya petroli yamepanda mara dufu, licha ya mzigo mzito unaozidi kulemea mlipa ushuru.

Kufuatia tangazao la Rais, wachangiaji wa mitandao walielekeza hisia mseto kwenye majukwaa ya mitandao.

“Kwa nini nyongeza hiyo iwafae wafanyakazi wa umma pekee?” Peter Wangodi akaandika katika Faceebok.

Naye Dave Idewa, kupitia mchango wake ametaka kujua wasio na ajira watafaidi vipi?

“Na kwa Wakenya wengi wasio na ajira Mtukufu Rais?” Idewa akasaili.

“Pesa za kupunguza gharama ya mafuta ya petroli na mbolea zilitoka kwanza? Tufahamishwe,” Silver Kipchumba akahoji.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta hata hivyo alisifia hatua ambazo serikali ilichukua 2020 na 2021 kuondoa na kupunguza ada na ushuru (VAT) kwa baadhi ya bidhaa muhimu za kimsingi.

“Kwa ground, nyongeza iliyotangazwa nina uhakika haitatekelezwa,” Oscar Ozil Njeru akaandika katika Twitter, naye Okoth wuod Okech akiuliza “Wenye hatuna kazi faida ni gani?”

“Hongera Rais wangu,” @Chizanodo msafiri akapongeza Rais Kenyatta.

@OtienoFelixOtienoz vilevile amesifia nyongeza hiyo
Wameongezewa Wale wachini tu,
 
Kama hawezi pandisha mishahara basi ashushe Kodi PAYE
 
Hv mishahara ikiongezeka unadhan wafanyabiashara hawatojua?????hili suala co siri kama mnavyotaka kuwaaminisha wengne
Mjomba hukusoma fasihi wewee, hakutaka kusema hadharani kumbuka enzi za mkapa alikuwa hatamki ovyo lakini mwezi july kitu kimesoma lengo ni kuzuia kupanda kwa bidhaa ovyo elewa basii sio lazima atamke ameongeza subiri july utaona wameongezwa au laaah!!
 
Hongera Rais leo wafanyakazi wameondoka na tabasamuuuuu
Unaweza kuta akaongeza elfu 20000,hapo ndo mtajua hamjui, kenya kaongeza 12% ya kile mtu anapata maana yake aliekua anapata mil MOJA anaongezewa laki na ushee ambayo ni sawa na m MOJA KWa pesa za kibongo , wakenya tuwaache wameisha tupiga gape, kuanzia katiba yao , nk
 
Unaweza kuta akaongeza elfu 20000,hapo ndo mtajua hamjui, kenya kaongeza 12% ya kile mtu anapata maana yake aliekua anapata mil MOJA anaongezewa laki na ushee ambayo ni sawa na m MOJA KWa pesa za kibongo , wakenya tuwaache wameisha tupiga gape, kuanzia katiba yao , nk
Kaongeza kima cha chini tu,
 
Back
Top Bottom