B Prosper
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 2,527
- 4,097
Hapo namtumbo gono limechachamaa balaa. Usisahau barakoa mkuuHuo mualiko unamsaidiaje maskini wa kule Namtumbo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo namtumbo gono limechachamaa balaa. Usisahau barakoa mkuuHuo mualiko unamsaidiaje maskini wa kule Namtumbo
Kufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Hassan atafanya ziara ya kitaifa tarehe 11 hadi 12 Februari, 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema lengo la ziara hii ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.
Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya elimu, afya, masuala ya amani na kiroho.
"Kanisa katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5," inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na kanisa katoliki.
Tofauti za udini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
=====
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis amemualika Rais Samia Suluhu Hassan Mjini Vatican kwa mazungumzo rasmi ya siku mbili baina ya viongozi hao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo kuwa mazungumzo hayo yatafanyika Februari 11 na 12 Vatican nchini Italia.
Makamba amesema kufuatia mwaliko huo, Rais Samia ameamua kuambatana na waumini wa kawaida wa Katoliki ambao pia wataonana na Papa Francis katika ziara hiyo ya kihistoria.
"Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu na Rais wetu, kwani mazungumzo hayo na Baba Mtakatifu ni ya heshima kubwa na watu wachache sana ndio watapata fursa ya kuhudhuria mazungumzo hayo," amesema Makamba
Nyie ndo mlikua mnatuletea Maneno aliyoongea Maghufuri na Mke wake, wakiwa wawili tu Chumbani.Kwako
Acha uongoNdie boss wao papa ana degree 33 kwa cheo
Magu Aliitwa na MUNGU akaja SAMIA 😀😀😀😀 SIO KIPYA HICHO MKUU?Hata angeitwa na Mungu hakuna kipya kingetokea
Ni kwasababu ndan ya kila serikali kuna watu waumini ya kikristo ambao ni ngumu kwenda kinyume nae kwa viapo vya imani.Ila Hawa Vatican Wana nguvu Gani? Papa anaweza hata kum summon Biden chap tu
Ila Hawa Vatican Wana nguvu Gani? Papa anaweza hata kum summon Biden chap tu
Sema katumia lugha ya kilaghai.Hiyo ni lugha ya kidipromasia waziri kaitumia wengi hamwelewi,
Maskin yeye anasaidiaje tajiri ??Huo mualiko unamsaidiaje maskini wa kule Namtumbo
Ingekuwa kule kwingine mgesema anatoa mrejesho kwa wajomba zake.Eti mazungumzo ya siku mbili 😆😆.
Biden kakaa kwa mazungumzo na papa kwa takriban dakika 75, hakuna kiongozi aliyewahi kuufikia muda huo.
Huyu wa kwetu siku mbili watakuwa wanajadili nini!
Halafu kaitwa hakualikwaIla Hawa Vatican Wana nguvu Gani? Papa anaweza hata kum summon Biden chap tu
Haunizidi ..Mimi mwenyewe mkristo mkatoliki ila nimepiga ngungi ukuta hapa yaaani... sijui katuroga nani kama Taifa.....aisee napatwa na hasira wakuu natamani hata kulia 😿😢😿
Ukweli ni kwamba ameomba kwenda kuonana na papa! Acheni kulemba lemba.Amealikwa au amejialika ,tuwekane sawa hapa , kama vipi leta ushahidi wa mwaliko , why mnachukulia watz wapumbavu sana nchi hii, kumbuka
Kikwete alijialika
Mkapa alijialika n.k ,so kipi cha msingi sana Papa amwalike ,Tueshimiane mtoa mada hauijui Dunia
Pope huwa halaiki viongozi wa nchi bali viongozi huimba kutembelea/kutembelewa na pope. Hiyo taarifa ya makamba ina uchawa ndani yakeKufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Hassan atafanya ziara ya kitaifa tarehe 11 hadi 12 Februari, 2024.