Nimewahi kuishi Moshi miaka mingi sana. Nawafahamu kwa kiasi fulani wachaga. Wakiwa mikoa mengine tofauti na kwao wachaga ni kama wamoja hivi lakini ukiwa kwao Kilimanjaro aisee hawa jamaa kila moja na kwao utasikia tu mimi mmarangu, mkibosho, mrombo, mmachame, mnarumu, muoldmoshi, muuru, msiha, mkiruwa n.k. Na kwa kiasi kikubwa hayo maeneo yote yana machifu/mangi/viongozi wao japo siku hizi hawana nguvu sana nje ya maeneo yao toka serikali ilipofuta hayo mambo ya machifu.
Maswali ya msingi hapa
1. Je hao mamangi/viongozi wa kila eneo walikaa lini na wapi wakakubaliana kuwa Mareale ndio mkuu wao?
2. Kuna kipindi si muda mrefu sana huyo Mareale alikuwa na kesi mahakamani na ndugu yake ya kugombea uchifu, je ilishaiisha na maamuzi
yalikuwaje
3. Na kama machifu wote wa Moshi walikubaliana kumualika mgeni rasmi mbona kwenye tangazo anatajwa tu Marealle kwa nini isiwe "chifu
mkuu Marealle kwa pamoja na machifu wenzake fulani na fulani wa Kilimnjaro wanamwalika mgeni rasmi ........... kwenye tamasha?
4. Shughuli nyingi za machifu huwa zinaambatana na shughuli za kishirikina na uganga wa jadi kwa kiasi fulani hili kila mtu anajua, je kwa mtu
ambaye ana imani na hofu ya Mungu kushiriki shughuli za hawa watu si kuchanganya mambo kweli?
Ni mtizamo tu.