Rais Samia achana na siasa za watemi na machifu, ni hatari, hazikusaidii na hazilisaidii taifa

Rais Samia achana na siasa za watemi na machifu, ni hatari, hazikusaidii na hazilisaidii taifa

Justification ya kipuuzi sana. Sijui kuwa kuna watu hapa JF wanaweza kuandika vitu vya kipuuzi namna hii.
1642878164915.jpeg
 
Huo ndio upofu wa kusoma mambo nusu nusus; Cheif marealle anayezungumzwa kwenye document la zamani hilo alifariki tangu mwaka mwaka 2007 akiwa na umri takriban miaka 92. Huyu anayeitwa Chief Marealle leo ni mmoja wa wajukuu zake tu, wala hajulikani zaidi ya hapo uchagani tu. Uksioma hayo madocument hayo ya zamani utakutana pia na jinsi walivyokuwa wanamhusudu Nyerere, hata alipokwenda kutembelea Uingereza, alipokelewa na malkia mwenyewe badala ya waziri mkuu!
 
Huyu mama anafikiri anajijenga kiasiasa kwa kukumbatia mambo ya kishirikina yaliyopitwa na wakati, zaidi ya kufanya uganga na matambiko machifu wana jambo gani la maana kwenye jamii ya watu waliostaarabika katika karne hii ya 21..........hivi leo tunaweza kuwatumia machifu kubuni chombo cha kwenda kufanya utafiti anga za juu, au watachekecha manyanga na matunguli yao na kurusha ungo kwenda sayari ya Mars........bwahahahaaa...........chifu hangaya bhana..​
Achana na hizo mambo za wazungu. Sisi huku tuendelee kuchawiana, kutoana mapepo, na kufanya sherehe, kula, kunywa, kucheza ngoma na mambo kama hayo.

Akili za viongozi wako hazina huo muda wa kuwaza mambo hayo. Hata ujenzi wa vyoo mpaka mzungu atume mpunga.
 
Atatuletea balaa. Huko tulishapita wala hatutaki kusikia machifu. Yuko desperate kutafuta political base. Nadhani 'reactionaries' wapinga maendeleo wanamshauri kwenye machifu. Uchifu unaambatana na desturi za imani za kishirikina umwinyi na kuleta ukabila na kunyanyasa wanawake. Hatutaki hiyo.
Hangaya hana uwezo kuongoza nchi hii. Ajitahidi tu ku maintain status quo hadi 2025 tuweze tafuta magufuli mpya.
Tumeona tayari yuko pro business people tofauti na desturi nchi hii tunataka kiongozi pro people... Maendeleo kwa umma sio watu wachache kuhodhi uchumi wa nchi kushirikiana na ubeberu wa kimataifa.
Amekwama Hangaya..
 
Tangu Rais Samia ashike madaraka amekuwa busy sana kuzing'ang'ania na kuzipigia debe siasa za kuwaenzi na kuuenzi utamaduni wa machifu na watemi hapa Tanzania. Hapa nitaweka kweli kadhaa kuhusu ubaya wa siasa hizo kwa nchi yetu na vizazi vijavyo.

1. Utamaduni wa watemi na machifu ni utamaduni wa kikabila na kikoo kwa 100%. Hawa hawafanani, hawakubaliani na hawakai chungu kimoja. Unalenga kuwagawa watanzania kuliko kuwaunganisha.

2. Utamaduni wa watemi na machifu umezungukwa na mfumo dume kwa karibu 100%. Kadri unavyopaliliwa ndivyo ambavyo mfumo dume unakuzwa na kuota mizizi kwenye jamii.

3. Kwa sehemu kubwa sana tamaduni za watemi na machifu zimejikita kwenye ubagani, matambiko, ushirikina na mambo ya kale. Sioni mantiki yoyote kwa serikali kuukumbatia sasa kwenye karne ya 21.

4. Kwa sehemu kubwa utamaduni wa tawala za machifu unakinzana na mifumo ya tawala rasmi za kiserikali na kisheria. Huwa ni vitu visivyoweza kwenda sambamba. Kuimarika kwa tawala rasmi za kiserikali automatically kuliua tawala za machifu na watemi, kuzifufua upya hizo tawala za machifu sasa ni kuhatarisha uwepo wa tawala rasmi za kisheria na kiserikali.

5. Utamaduni wa tawala za watemi na machifu kwa sehemu kubwa umedhoofika, kufifia, kuparaganyika au ulishakufa kwa jamii nyingi sana hapa Tanzania. Wengi watakaoibuka sasa na kuitwa watemi au machifu huenda watakuwa waganga wa kienyeji, wazee wa kikoo, matapeli (wazee wa fursa), wajumbe wa CCM wa nyumba kumi kumi (wazee wazee). Kiuhalisia utakuta sio watu halisi wa kuwakilisha watemi na machifu wa zama zile. Kuwakumbatia watu wa namna hiyo ni kupoteza muda na rasimali.
Toka lini tumeanza kuwapa nafasi wapiga ramli????
 
Back
Top Bottom