Rais Samia achana na siasa za watemi na machifu, ni hatari, hazikusaidii na hazilisaidii taifa

Mungu ni dhana na shetani ni dhana. Usifungwe na utamaduni wa kimagharibi. Hata sisi tunaweza kuwa na mungu wetu siyo lazima huyo mungu aliyeletwa na wazungu na wewe ukakalilishwa bila kujua
Tunaambiwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu hivyo wewe amini tu huyo mungu wako haina shida na mimi nitamwamini ninayemwamini. Upo hapo..?
 
Acha tuone huenda Chifu hangaya ana maono yake....
 
Mimi ninavyoelewa Mungu ni moja na ndiye aliyeumba vyote vilivyomo katika dunia hii, mimi siamini kama kuna Mungu wa wazungu na Mungu wa waafrika, kwa kifupi siamini ktk uwepo wa hao miungu unaosema.
Kabla ya wazungu kuja wazazi wako walikuwa wanaabudu mungu yupi
 
Acheni kumtukana Magufuli nchi itatulia, vinginevyo tunaelekea kuwa sawa na watu wa Babiloni
 
Jamani muacheni ajaribu anacho jaribu majibu atayapata baadae...
Hili taifa sasa hivi kila mtu anajaribu kitu chake hata walivyo ambiwa wasijaribu wanajaribu... Wacha wajaribu
 
Wakulaumiwa ni washauri wake. Hii ni ku balcanise
Chief Marialle huwa analetewa fedha kutoka kwa Malkia Elizabeth wa Uingireza.
Hivyo kitendo cha samia kuungana naye kuna upigaji mkubwa wa fedha kutoka UK. Na picha zitatumwa UK nyingi sana Leo
Hii Balkanisation/Kutugawa Kikabila ni hatari sana. Ila wa kulaumiwa ni WASHAURI wake maana wanampotosha.
 
Machifu walikuwa kwa sehemu kubwa vibaraka wa ukoloni. Wengi pia walitawala kwa mifumo ya kitapeli, kiwiziwizi, unyanyasaji, udikteta, uporaji nk.
Kuuza wanajamii yao kwa wakoloni.

Museve, suala la Machief lilitaka kumuweka matatani! Huko west Uganda watu wakawa hawaogopi risasi za polisi kisa Chief kaagiza. Ili mlazimu Museveni kumuamisha chifu huyo nankumuweka kwenye kind of house arrest!!!

Machief....tuna wapenda lakini wana taabu zao.
 
Ulipotaja Magufuli ndo ulipoharibu, kwa dunia ya wasitaarabu na yenye usitawi haiwezi kulilia kuongozwa na sadist Kama JPM. Taja mwingine plz, Kama Taifa tulikosea sana awamu ya tano, na Mungu akaamua kutuponya, usiturejeshe huko.
Umeona eh watu wengine badala ya kumshukuru Mungu tena wanakumbushia machungu,hii ni ajabu kabisa.
 
Anataka aweke legacy ya kurudisha uchifu, pia tunamuomba kule Zenj arudishe usultan.
 
Chief Marialle huwa analetewa fedha kutoka kwa Malkia Elizabeth wa Uingireza.
Hivyo kitendo cha samia kuungana naye kuna upigaji mkubwa wa fedha kutoka UK. Na picha zitatumwa UK nyingi sana Leo
Dah kumbe bibi anatuma mzigo kwenye koloni lake? Hapo sawa
 
Wakati mwingine ifike mahali wasaidizi wa SSH wasimhusishe na watu wa ajabu..
Huyu anayejiita Mangi Mkuu wa Wachaga si ndiye aliyeupora umangi kutoka kwa ndugu yake?
Si ndiye aliyenunua mahoteli kibao kwa mgongo wa uwekezaji kisha akayafunga? Embassy Hotel - Dar etc..
 
Hizi siasa za kukumbatia viongozi wa kimila hazina tija kwa nchi yetu zama hizi.....kuna sehemu tunafeli tunapoendekeza hui usanii
Wanaoandaa events za Rais wajitahidi sana ili isionekane kuwa Rais anatafuta support ya wadau.

Kwasababu inaonekana kabisa kuwa haya ni maandalizi ya 2025.

Anyways. Namtakia kila la heri Madam President.
 
Huyu mama anafikiri anajijenga kiasiasa kwa kukumbatia mambo ya kishirikina yaliyopitwa na wakati, zaidi ya kufanya uganga na matambiko machifu wana jambo gani la maana kwenye jamii ya watu waliostaarabika katika karne hii ya 21..........hivi leo tunaweza kuwatumia machifu kubuni chombo cha kwenda kufanya utafiti anga za juu, au watachekecha manyanga na matunguli yao na kurusha ungo kwenda sayari ya Mars........bwahahahaaa...........chifu hangaya bhana..​
 
Divide and rule; katika karne ya ishirini tupande basi la ukabila !
 
Chief Marialle huwa analetewa fedha kutoka kwa Malkia Elizabeth wa Uingireza.
Hivyo kitendo cha samia kuungana naye kuna upigaji mkubwa wa fedha kutoka UK. Na picha zitatumwa UK nyingi sana Leo
Justification ya kipuuzi sana. Sijui kuwa kuna watu hapa JF wanaweza kuandika vitu vya kipuuzi namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…