Kiufupi hiyo ni WAKE UP CALL, mama asiposhituka hapa 2025 hatoboi. Yani jinsi hali ilivyo kwa wafanya biashara ndivyo hali hiyo ipo kila sekta kama kilimo, elimu, nk. Wafanyabiashara wanagoma kwani hakuna wa kuwatisha kwani mitaji ni yao. Watumishi wangekuwa walishagoma zamani ila vitisho vya kufukuzwa kazi ndivyo vinawafanya wakose ushirikiano. Kuna kundi la vijana tusio na ajira tupo wengi, hadi mwezi wa nne tukadanganywa eti mama ametoa kibali cha ajira za ualimu 2023/2024. Hadi leo hii hola! Mama asipokubali kushughulikia hizo changamoto kisawasawa basi 2025 atapata tabu kushawishi watu wamwelewe!