Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Uh - Oh!

Kafulila kakanyaga waya!

EeeeenHeeeee!

Kelele zote zimeishia ukingoni? Usichezee waliopangwa, utapanguliwa tu!
Daah! Itakuwa kawashughulika wasiogusika wakati yeye hana vinasaba vya sisiemu. Miezi michache tu rais alimsifia, leo hii anapigwa chini.

Hii ni awamu ya kujineemesha, ukishika mikono ya wanaoneemeka unatumbuliwa.
 
CCM wanajuana, si ajabu baada ya muda tukamuona tena kwenye system kama ilivyokuwa kwa Chalamila.
 
Hizi kazi za uteuzi ni mtihani kwa kweli, inatakiwa ukiipata tu uweke mambo yako kwenye mstari, inakuwa ni kama kuishi na kusubiria kifo, inatakiwa usali na kuomba kila wakati, kwani haujui siku wala saa kifo kitakapokujia...
 
Anahitajika makuu ya JWTZ, kumbuka kuna Majenerali wamestaafu na wengine wametuliwa ubalozi na wengine wamepandiashwa vyeo hivyo wanaenda kuziba nafasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…