Katika mkeka huu mpya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng Robert Gabriel, Kafulila, Mtaka hawa naona hawakupaswa kuondolewa.
Mfano Ndg Gabriel aliweza kuunganisha makundi mengi mwanza hata Ushirikiano wake na Kanisa kanda ya ziwa ulikuwa ni wa kiwangi cha juu na heshima kubwa. Hapa ccm wametoa boko.
Mwanza hata Mongela hakupaweza alikuwa na maneno mengi matendo machache.
Huyu Fatma Mwasa hakustahili kupewa tena ukuu wa mkoa wala wilaya ni aina fulani ya viongozi wanaoangalia zaidi maendeleo yao binafsi na kuna tuhuma za ufisadi zikitajataja.
Mama yetu (umri wa kustaafu umefika)Halima Dendego mwanae Gift Msuya ni Ded moshi huko mama naye unakuja unampa ukuu wa mkoa lakini ana historia ya ndani na ccm top cream asingeweza kuachwa na baadhi ya hizi teuzi mama anapewa majina inavyoonekana kutoka Lumumba.
Ccm wana tabia ya kurecycle watu wale wale wengine hawaja accomplish chochote kama common names Batilda buriani,
Kwa wajeda wale nadhani iko shida ya management ya wajeda kwa civilian nimeshangaa sana Mjeda wa mtwara with his knowledge katika zama za citizen journalism na teknolojia iliyojaa tele anamtafuta aliyepiga picha ajali ya school bus. Siku hizi ukidondoka unaeshangaa picha zako zimeene magroup kibao ya wasap pasipo kujua mpiga picha nani. Kuna tatizo kwenye elimu yetu na mitaala kwa kweli.