Rais Samia afanya uteuzi na mabadiliko madogo ya vituo vya kazi

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Me. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:

Amemteua Bw. Tito Philemon Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe; na

Amemteua Bw. Mussa R. Kilakala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.

Aidha, Mhe. Rais amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kama ifuatavyo:-

Bw. Athumani Francis Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga;

Bi. Mwantum Hamis Mgonja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji; na

Bi. Mwamvua Bakari Mnyongo kutoka Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma.
 
Reactions: Lee
Kwa hyo alishindwaje kuunganisha na zile za jana. Attention seeking idiot
 
Udini mtupu na uzanzibar
 
Leo ijumaa twendeni tukaswali walioteuliwa. Ni wengi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…