Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Chadema wameangukia pua tena.

Chama hiki kina laana
Waliwaombea njaa Hapi na Chalamila wakidhani mama atawafurahisha kama alivyowafurahisha kwa Ole Sabaya wakajisahau zile shangwe kuwa zitamshtua mama,ukiona mbaya wako anashangilia maamuzi unayoyafanya jua kuna kasoro na hayo maamuzi.
 
Wanyarwanda Ngara na Biharamuro waliifanya mali yao zama za JK. Kila siku walikuwa wanauwa watanzania huko na kuingiza mifugo kama kwao.

Magufuli akapiga stop huo upuuzi, watanzania tunasahau haraka sana changamoto zilizokuwa za kawaida katika baadhi ya maeneo kabla ya Magufuli.
Wanajeshi huko wameanza kupelekwa hata kabla ya mwendazake mkuu....Toka enzi za kina Kanali Massawe pamoja na wilaya za Kigoma kule alikoenda kuharibikiwa Mkisi

Sio mambo ya JK na JPM ni hali ya mipaka yenyewe ilivyokua
 
Dar es salaam tupo na Pedeshee Amos Makalla na baba Gabriel.
 
Naendelea kujifunza Jambo tokea teuzi za nyuma hadi za huyu mama, ukoo ni uleule na system ni ile ile. Sio rahisi kuondoa mfumo fulani na watu wake wote na nchi ikaendelea. Nafikiri wapiga kelele mitandaoni mtaendelea kujifunza jambo
 
Kula kiongozi na jeshi lake mwana,huwezi kuongoza kwa jeshi la mwengine.Huyu sio magu na wala haongozi kama magu.na waru kama nyie mnaotaka umagu uendelee inabidi mbadirike,sasa kama angeaacha kila kiongozi alipo alafu hao viongozi wakafa ingekuwaje?!.Sifa kubwa ya kiongozi ni kuweza kurithisha wengine anachofanya ili akiondoka aloyaacha yaendelee.Enzi za magu kila kitu ilikuwa ni yeye ndo maana alivoondoka watu wanachanganyikiwa,mwacheni mama apige kazi anavyoweza.
#kaziiendelee. Panga safu mama.
Magufuli hakuwa perfect busara ni kuondoa yasiyofaa na kuiga yenye faida.

Uongozi mpya aina basi raisi anaanza upya admin ya serikali ni going concern majukumu yake yapo pale pale ata raisi angekuwa anatokea upinzani.

Kama mtu wa aina fulani alihitajika kwa sababu ya changamoto husika katika eneo fulani basi mwenye weledi ule ule anahitajika katika ilo eneo raisi awe Samia, Magufuli, Mbowe, January, Mtaka au hata ingekuwa wewe.

Ndio alichofanya Magufuli katika baadhi ya maeneo na kuacha watu kwa muda mrefu kwa sababu walishapata uelewa wa maeneo yao.
 
Uteuzi wa Dar na Dodoma nimeupenda.
Kweli kama ipo ipo tu Makala tulishaanza kumsahau,ila jamaa kama ni mganga kweli kampata ,akikosa huku anapelekwa kule akikosa kule anarudishwa huku. Kweli mtoto wa mujini ni wa mujini tu.
 
Makonda alikuwa na skills gani akawekwa Dar? Hakuna watu walikuwa wanaufahamu mkoa wa Dar zaidi yake?
Mama ilimradi tu afanye lolote aongolewe kwa miaka watu walikuwa wanalalama kubadilisha badilisha wakuu wa mikoa na wilaya kunaondoa consistencies ndio maana Magufuli aliwaacha.

Hao watu kwa muda waliokaa wanafahamu changamoto za maeneo yao, plan zilizokuwepo na changamoto za watendaji wao.

Kingine Magufuli for once alijitahidi kuweka wakuu wa mikoa kutokana na maeneo wanayoyafahamu au skills zao ili watatue changamoto kutokana priority wanazozifahamu wao.
 
Amos Makala alikuwa bench sio,
kitabo alikuwa Rukwa.
safi sana sasa apige kazi kweli kweli.

Mkoa wa Dar unataka mtu makini sana na mfuatiliaji, bila kusahau ukali ni muhimu inapo bidi.
nginja ngija......
Hajawahi kuwa Rukwa. Alikua mbeya akapelekwa Katavi akashindwa kuuza vitambulisho vya wamachinga ndo kaenda Bench naona kakumbukwa

Alivyotoka Katavi ndo Kamuachia huyo kijana Homera aliyekua makao makuu CCM then DC wilaya moja huko mkoa wa Ruvuma sikumbuki vizur

Mbeya na Katavi naona kama Zinabadilishana RCs😂😂

Anarudi mjini Pedeshee
 
Back
Top Bottom