Rais Samia afungua Shule ya wasichana Tanga, apendekeza iitwe Beatrice Shellukindo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia akifungua shule ya wasichana Tanga Februari 25, 2025.


Rais Samia amependekeza Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Kilindi iitwe jina la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilindi kupitia CCM Beatrice Shellukindo aliyefariki Julai, 2016.

Rais Samia amwagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi kupeleka Kliniki ya masuala ya Ardhi Kilindi ili kushughulikia migogoro ambayo pia inasababishwa na viongozi wa sehemu husika.

Rais Samia ameahidi kutoa Genereta na Gari katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kilindi (Beatrice Shellukindo) na amesisitiza Wanafunzi kuacha ya dunia na kuwekeza nguvu kwenye masomo zaidi.
 
Akiwa katika muendelezo wa ziaa yake huko Tanga,Rais wa JMT amezindua shule Mpya ya Wasichana ya Mkoa mchepua wa Sayansi iliyojengwa Wilayani Kilindi.

Katika kuenzi mchango wa Wanawake,Rais amependekeza shule hiyo Kuitwa Beatrice Shelukindo.

View: https://www.instagram.com/p/DGfbjsGKfeT/?igsh=cjdnOWZlbzQ1M3Ax

My Take
Hii ni Kati ya Shule 26 za High School maarufu kama shule za Samia alizojenga maalumu Kwa Ajili ya kumuinua mtoto wa kike Kila Mkoa.

Kazi inaendelea Kwa shule za Wavulana pia.Mi 5 tena Kwa SSH.

View: https://www.instagram.com/reel/DGfTiFSAHcu/?igsh=ZDJ1ZjhhcXl0Y2ho
 
Nguvu ya haya majina yanasaidia sana Chama kutawala,majina yana viapo na maagano,ndio maana yule simba kulee ng'ambo ya maji aliitwa jina la msingida,simba aliyefungwa na hatoki kwenye uzio wake.Mnanipata!!?kiroho zaidi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akifungua Shule ya Sekondari ya wasichana Tanga iliyopo Mabalanga katika Kijiji cha Michungwani Wilaya ya Kilindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 25 Februari, 2025.
 

Attachments

  • FB_IMG_1740542178164.jpg
    FB_IMG_1740542178164.jpg
    74.3 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740542175211.jpg
    FB_IMG_1740542175211.jpg
    72 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740542173118.jpg
    FB_IMG_1740542173118.jpg
    101.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740542170796.jpg
    FB_IMG_1740542170796.jpg
    100.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom