Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Zifutwe maisha
Badala yake labda muwe na bank holiday tu
Sherehe ni matumizi mabaya ya fedha na hazina tija yoyote na hazileti ajira wala chakula
 
Watanzania hawana cha kusherehekea. Walimtoa muingereza, leo wanatamani aheri muingereza angerudi. Muingereza hakuwa na utaratibu wa kuteka na kuua wapinzani kama huyu mkoloni mweusi wa sasa. Nyerere hakuwahi kutekwa Aliachwa aende mpaka umoja wa mataifa. Hawa wa sasa wangemteka pale airpot.

Tarehe 9 December ibadilishwe, badala ya kuwa siku ya sherehe, iwe siku ya huzuni kuu, maana ndipo nchi ilitoka kwenye ukoloni mwepesi, na ikaingia kwenye ukoloni mbaya kabisa, ukoloni wa shetani, ambaye siyo tu anapora rasilimali bali anaondoa roho za wanaomkemea.
Uhuru uko wapi kwanza watu wanatekwa kila kikicha kama Chile 🇨🇱 ya Agusto Pinochet
 
images.jpeg
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
angefuta safari zake nyingi zile na crew hadi ya kina stiveake na watu wasio na mchango wowote kwenye taifa hili. safari zile zinakula hela kuliko hata kumbukumbu ya uhuru wetu. mnapigwa changa la macho la kisiasa mshaona mtu kafanay la maana.
 
Serikali yetu inatakiwa ibane matumizi kadiri inavyo wezekana. Nchi yetu bado watu wake ni masikini.
Viongozi kuweni na huru baneni matumizi.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Zanzibar mbona mapinduzi day haifutwagi?
 
Hivi Kuna nchi ilipata uhuru iliyokuwa inaitwa Tanzania Bara?
Yaani nashindwa kuelewa kwanini kusema uhuru wa Tanganyika unaonekana kama mhaini unataka kupindua nchi sasa viongozi wakubwa wa juu kama hawa wanaogopa kusema Tanganyika then wanasema uhuru wa Tanzania bara,sielewi kwanini wanataka kulifuta jina la Tanganyika kwenye history ya hii nchi ya Muungano na kwa masilahi ya nani.
 
Kwa nini bajeti yake ilitengwa?? Hyo bajeti isiwe inatengwa.
 
Back
Top Bottom