Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Siku za uhuru kuna marudio ya matukio yale yale ya kila mwaka, wanapoamua kuahirisha wanakuwa wameshapima hasara zozote (kama zipo) zinazoweza kutokea baada ya kufanya hayo maamuzi...Ni taifa la ajabu lisiloenzi uhuru wake.
Ni masuala yale yale ya makomandoo kuvunja mawe vifuani mwao na zile show za kutua na kamba kutoka kwenye helikopta.
Wajanja wanapiga pesa kupitia bajeti zinazotengwa kwa ajili ya shughuli zote za halaiki za siku ya uhuru.
Najua umeamua kupinga kwa sababu ni maamuzi ya Rais Samia ambaye upo uwezekano haumpendi, kwa hiyo unapinga sio kwa sababu unaipenda sana siku ya uhuru bali ni siasa tu za chuki.