Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Next time afute pia sherehe za Muungano! Maana huo Muungano wenyewe hauna tija yoyote ile kwa Tanganyika! Zaidi tu unaendelea kuwanufaisha Wazanzibari.

Lakini pia afute yale matamasha ya Kizimkazi! Na fedha zitakazo okolewa zipelekwe kwenye vikundi vya akina mama wanaohangaika na mikopo ya kausha damu.

Afute pia na zile mbio zao za mwenge! Na zenyewe zinatafuna tu kodi zetu kwenye hii dunia ya utandawazi.

Halafu ajitahidi kujizuia na ziara zake zisizoisha za nje ya nchi! Ikiwezekana aanze na kuahirisha kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mwanamke wa Namibia. Na hela zitakazo okolewa, atutumie vocha kwenye namba zetu za simu.
 
Hizi headline huwa mnazitoa wapi,mbona sijasikia Waziri Mkuu akisema amefuta sherehe.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Hivi kati ya Sherehe za Uhuru na mbio za mwenge kipi muhimu kwa historia ya nchi yetu? Ni mwaka gani mbizo za mwenge ziliwahi kufutwa/kuahirishwa?
 
Watanzania hawana cha kusherehekea. Walimtoa muingereza, leo wanatamani aheri muingereza angerudi. Muingereza hakuwa na utaratibu wa kuteka na kuua wapinzani kama huyu mkoloni mweusi wa sasa. Nyerere hakuwahi kutekwa Aliachwa aende mpaka umoja wa mataifa. Hawa wa sasa wangemteka pale airpot.

Tarehe 9 December ibadilishwe, badala ya kuwa siku ya sherehe, iwe siku ya huzuni kuu, maana ndipo nchi ilitoka kwenye ukoloni mwepesi, na ikaingia kwenye ukoloni mbaya kabisa, ukoloni wa shetani, ambaye siyo tu anapora rasilimali bali anaondoa roho za wanaomkemea.
Unawazungumzia watanzania gani? Mbona uyasemayo hayaakisi watanzania wenyewe...
Alafu unataka serikali ifanye nini kwa wanaojoteka wenyewe??
 
..mama ndiye mwenye nongwa mpaka kafuta sherehe za uhuru. Mbona za Mapinduzi hazijawahi kufutwa?
Sio mara ya kwanza nchi hii hizo sherehe kufutwa, hayati Magufuli alizifuta mwaka 2015, mliwahi kumuuliza kwanini zile za mapinduzi hakuzifuta?.
 
Hivi amefuta au ameelekeza namna tofauti ya kusherehekea tofauti na ile iliyozoeleka ya magwaride?
Ila Kiswahili kigumu sana.
Uzi kama huu unaandikwa na watu wa ule upande wa Luhaga Mpina, wanaojiona wanajua kila kitu kumbe yapo mengi ambayo hawayajui.

Samahani kama nakera watu humu jamvini, wasukuma wanasumbuliwa sana na superiority complex.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
IMG_7633.jpeg

IMG_7632.jpeg

Hivi tunaelewa hata symbolism ya hizo poppy seeds

If only you knew the efforts that goes behind to ensure that day is special nationally.

You think it’s easy
 
You think nationalism propaganda is an easy task.

Ndugu usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili.

It’s not a joke civil services za hao watu hazina watu wa mzaha-mzaha.

Kazi ya kuendesha nchi sio shughuli kama sisi tunavyofikiria.

Not a joke at all
 
Kuhusu Mwenge wa Uhuru? Kwa nini usifutwe na gharama za kuukimbiza nchi nzima zisaidie/ziboreshe huduma za kijamii?
 
Hili nalo langoli aachane nalo. Halina faida.
Tutafute mfumo bora kiasi cha kwamba pale timu youote inawakilisha nchi katika mchezo wowote ule serikali inagharamia flights na accomodation. Timu husika ilipe mishahara na hizo bonus za magoli.
kabisa ndugu
 
Lengo lilikuwa zuri, pesa ilipelekwa kwenye sekta nyingine na ndio kitu anachokwenda kukifanya Rais Samia safari hii.

..uhuru lazima uenziwe na kusherehekewa.

..wananchi lazima wajitambue nafasi yao na wajivunie utaifa wao.

..uhuru na utaifa ni mambo makubwa kuliko pesa, na vitu.

..siku ya uhuru na mashujaa kwa maoni yangu ni lazima ziadhimishwe.
 
Umeandika nadharia tupu mkuu, Rais anaitazama kazi yake katika mtazamo tofauti na haya mawazo yetu yenye kufanana na maongezi ya viti virefu vya Bar na katika mabenchi ya mafundi viatu wa mitaani.
 
Kinachofanyika ni kuuwa kabisa fikra za uhuru wa Tanganyika kwa vizazi vijavyo. Ikiendelea namna hii miaka mitano changanya na kizazi cha simu, game na mpira tutakuja kuambiwa HISTORIA ya ajabu.
 
Umeandika nadharia tupu mkuu, Rais anaitazama kazi yake katika mtazamo tofauti na haya mawazo yetu yenye kufanana na maongezi ya viti virefu vya Bar na katika mabenchi ya mafundi viatu wa mitaani.

..Ni taifa la ajabu lisiloenzi uhuru wake.
 
Back
Top Bottom