Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Next time afute pia sherehe za Muungano! Maana huo Muungano wenyewe hauna tija yoyote ile kwa Tanganyika! Zaidi tu unaendelea kuwanufaisha Wazanzibari.Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.
Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.
Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".
Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.
"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Lakini pia afute yale matamasha ya Kizimkazi! Na fedha zitakazo okolewa zipelekwe kwenye vikundi vya akina mama wanaohangaika na mikopo ya kausha damu.
Afute pia na zile mbio zao za mwenge! Na zenyewe zinatafuna tu kodi zetu kwenye hii dunia ya utandawazi.
Halafu ajitahidi kujizuia na ziara zake zisizoisha za nje ya nchi! Ikiwezekana aanze na kuahirisha kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mwanamke wa Namibia. Na hela zitakazo okolewa, atutumie vocha kwenye namba zetu za simu.