Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Uhuru uko wapi kwanza watu wanatekwa kila kikicha kama Chile 🇨🇱 ya Agusto Pinochet
angefuta safari zake nyingi zile na crew hadi ya kina stiveake na watu wasio na mchango wowote kwenye taifa hili. safari zile zinakula hela kuliko hata kumbukumbu ya uhuru wetu. mnapigwa changa la macho la kisiasa mshaona mtu kafanay la maana.Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.
Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.
Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".
Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.
"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
magufuli alikuwa vizuri sana kwenye kubana matumizi. safari moja tu ya samia inagarimia shilingi ngapi?Serikali yetu inatakiwa ibane matumizi kadiri inavyo wezekana. Nchi yetu bado watu wake ni masikini.
Viongozi kuweni na huru baneni matumizi.
Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".
Zanzibar mbona mapinduzi day haifutwagi?Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.
Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.
Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".
Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.
"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Yaani nashindwa kuelewa kwanini kusema uhuru wa Tanganyika unaonekana kama mhaini unataka kupindua nchi sasa viongozi wakubwa wa juu kama hawa wanaogopa kusema Tanganyika then wanasema uhuru wa Tanzania bara,sielewi kwanini wanataka kulifuta jina la Tanganyika kwenye history ya hii nchi ya Muungano na kwa masilahi ya nani.Hivi Kuna nchi ilipata uhuru iliyokuwa inaitwa Tanzania Bara?
Ni mabilioni kadhaaHivi ile kizimkaz festivo bajet yake mliipata!
Futa na hizo samia marathon sjui samia blah blah zote hizo ni njiaa za kupiga tu
Ova
HaipoHivi Kuna nchi ilipata uhuru iliyokuwa inaitwa Tanzania Bara?
Kuna lile dude washa linaitwa Mwenge lile!Hii akili. Mie nadhani tungekuwa tunasherekea kila baada ya decade tuu