Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza kwa njia ya "video" na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Michezo katika Kanda ya IV ya Afrika (AU Sports Council of Ministers Meeting – Region IV) unaofanyika Jijini Arusha hapa Tanzania.
Rais Samia amepiga "kimombo" kilichonyooka kwelikweli, msikilize hapa akiwashukuru wawakilishi wa Mataifa yanazoshiriki mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Rais Dkt. Samia Amewasilisha ujumbe maalumu kwa wajumbe na Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV.
“Niwahakikishie kuwa Tanzania ina uzoefu wa kuwa makao makuu ya taasisi mbalimbali za kimataifa, na pia Tanzania ina miundombinu yote muhimu ambayo itaiwezesha baraza hilo kufanya kazi kwa ufanisi” Amesema Rais Samia.
Vilevile Rais Samia amewasihi wajumbe wa mkutano huo kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii ya Tanzania ili kujionea namna nchi yetu ilivyobarikiwa.
Rais Samia anaimarisha na kuboresha kama sio kurejesha tena nchini utalii wa mikutano pamoja na kutoa nafasi kwa utalii wa michezo.