Rais Samia aitwe na kutambuliwa kama Mama wa Taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu watanzania,

Nashindwa nianze na lipi juu ya kumuongelea Rais huyu shupavu, Hodari, Mahiri, mnyenyekevu,mwenye moyo wa upendo,huruma na ukarimu, Msikivu na mwenye Subira, madhubuti na Imara, mwenye msimamo na asiye yumba, mwenye Dira na muelekeo sahihi, mwenye Sera na ajenda za kugusa maisha ya watanzania, Aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania wote, Mwenye upendo wa dhati na watanzania na Taifa lake na anayetumia muda wake mwingi kuzungumza na kuwatumikia watanzania.

Ni kiongozi wa aina yake na mfano wa kuigwa Barani Afrika, Ni Hazina kwa Taifa letu, Ni msingi wa amani na umoja wa Taifa letu, Ni nguzo ya umoja wa kitaifa na mshikamano wetu,Ni mwamba usio tikisika na ngome iliyo imara,Ni Rais kweli kweli aliye jaliwa kalama ya uongozi na Mwenyezi MUNGU,Ni kiongozi mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU ,mwenye kuhubiri na kutenda haki kwa matendo.

Ni kiongozi anayetazamwa na watu wa vyama vyote,Dini zote,makabila yote,jinsia zote,Rangi zote,Rika zote na Kanda zote Kama kiongozi wao na mlezi wao,Kila mmoja anampenda na kumheshimu Rais Samia,kila mmoja anamuunga mkono na kusimama Naye katika nyakati zote, Rais Samia Ni kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania wote, Nikiongozi aliye na uungwaji mkono kutoka katika makundi yote.

Hii inatokana na ukweli kuwa Rais Samia amekuwa akiwasikiliza na kumsikiliza kila mtu,Sauti zote za watanzania na mtu mmoja mmoja Zina nafasi katika masikio ya Rais Samia na macho yake, kila mtu Anayo nafasi katika ujenzi wa Taifa letu na kila mmoja anajiona Anayo nafasi katika ustawi wa Taifa letu kwa kuwa Rais Samia ametoa nafasi hiyo kwa kila mmoja wetu mwenye uzalendo na Taifa letu kutoa mchango wake katika ujenzi wa Taifa letu.

Hatua ya Leo ya kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa inatokana na dhamira yake njema katika ujenzi wa Taifa letu na kutambua mchango wa kila mmoja wetu kuijenga nchi yetu pamoja na kutaka kuona Taifa letu likiwa moja na kusonga mbele kwa pamoja bila kujari itikadi zetu za kisiasa, Rais Samia anahitaji kuona mafanikio tunayoyapata kiuchumi yanakuwa yetu sote na sote tujione kuwa sehemu ya mafanikio hayo na kuwa na mchango wetu katika kuyafikia.

Hataki kumuucha mtu nyuma Wala kumpuuza mtu au watu Wala kuzima sauti za watu fulani,anataka kusikia sauti za watu wote na maoni yao ili watu wawe na amani katika mioyo Yao, Hataki watu wajaze hasira na chuki katika mioyo Yao, Hataki watu wavimbe vifua vyao kwa vinyongo Bali anataka wazungunze kwa heshima, staha, uungwana, busara, upendo,uzalendo wa yale yaliyo ndani Yao na wanayofikiri kuwa yanaweza kuwa na mchango katika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu.

Ndio maana nasema kwa namna Rais Samia anavyokubalika na watu wote wa makabila yote,wa vyama vyote,Dini zote,Rika zote ,jinsia zote, makabila yote, hakika Anastahili kuitwa mama Wa Taifa letu. Anastahili na sioni Cha kuwa kikwazo ambacho unaweza kusema hiki kinamnyima fursa hiyo. Anastahili kwa kuwa ameonyesha uzalendo alio nao ndani ya moyo wake ambao muda wote amaelitaguliza mbele Taifa letu.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Amekataa chawa,Nani alifunga hiyo mikutano ,huyu ni dictator anayeendeleza kukanyaga katiba yetu ,ilitakiwa agombee msamaha Kwa kuwanyamazisha watanzania
Acha bla blaa,Akuombe msamaha Kama Nani na kwa kosa gani alilo lifanya Akiwa Kama Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama?
 
Moderador fanyeni mpango tuwe tunaweza kumpiga mtu vibao hukohuko aliko.
Yaani mikutano iziwiliwe na ccm na ccm hiyohiyo ifungue halafu isifiwe.??

Mama wa taifa atabaki kua mmoja tu Mama Maria Nyerere!❤️
Embu uwe na moyo wa shukurani kwa kazi kubwa na ya kipekee aliyoifanya mh Rais
 
Hongera Chawa wa Mama. Kiukweli kazi unaifanya. Sema tu ndiyo hivyo; bado hujakumbukwa.
 
Tatizo huelewi title ya mama au baba wa taifa hutolewa kwa sababu ipi...
 
Bila kubadili mfumo wa UTAWALA wa nchi hii, haya yote ni danganyatoto tu.
 
Ndugu zangu watanzania,

Nashindwa nianze na lipi juu ya kumuongelea Rais huyu shupavu, Hodari, Mahiri, mnyenyekevu,mwenye moyo wa upendo,huruma na ukarimu, Msikivu na mwenye Subira, madhubuti na Imara, mwenye msimamo na asiye yumba, mwenye Dira na muelekeo sahihi, mwenye Sera na ajenda za kugusa maisha ya watanzania, Aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania wote, Mwenye upendo wa dhati na watanzania na Taifa lake na anayetumia muda wake mwingi kuzungumza na kuwatumikia watanzania.

Ni kiongozi wa aina yake na mfano wa kuigwa Barani Afrika, Ni Hazina kwa Taifa letu, Ni msingi wa amani na umoja wa Taifa letu, Ni nguzo ya umoja wa kitaifa na mshikamano wetu,Ni mwamba usio tikisika na ngome iliyo imara,Ni Rais kweli kweli aliye jaliwa kalama ya uongozi na Mwenyezi MUNGU,Ni kiongozi mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU ,mwenye kuhubiri na kutenda haki kwa matendo.

Ni kiongozi anayetazamwa na watu wa vyama vyote,Dini zote,makabila yote,jinsia zote,Rangi zote,Rika zote na Kanda zote Kama kiongozi wao na mlezi wao,Kila mmoja anampenda na kumheshimu Rais Samia,kila mmoja anamuunga mkono na kusimama Naye katika nyakati zote, Rais Samia Ni kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania wote, Nikiongozi aliye na uungwaji mkono kutoka katika makundi yote.

Hii inatokana na ukweli kuwa Rais Samia amekuwa akiwasikiliza na kumsikiliza kila mtu,Sauti zote za watanzania na mtu mmoja mmoja Zina nafasi katika masikio ya Rais Samia na macho yake, kila mtu Anayo nafasi katika ujenzi wa Taifa letu na kila mmoja anajiona Anayo nafasi katika ustawi wa Taifa letu kwa kuwa Rais Samia ametoa nafasi hiyo kwa kila mmoja wetu mwenye uzalendo na Taifa letu kutoa mchango wake katika ujenzi wa Taifa letu.

Hatua ya Leo ya kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa inatokana na dhamira yake njema katika ujenzi wa Taifa letu na kutambua mchango wa kila mmoja wetu kuijenga nchi yetu pamoja na kutaka kuona Taifa letu likiwa moja na kusonga mbele kwa pamoja bila kujari itikadi zetu za kisiasa, Rais Samia anahitaji kuona mafanikio tunayoyapata kiuchumi yanakuwa yetu sote na sote tujione kuwa sehemu ya mafanikio hayo na kuwa na mchango wetu katika kuyafikia.

Hataki kumuucha mtu nyuma Wala kumpuuza mtu au watu Wala kuzima sauti za watu fulani,anataka kusikia sauti za watu wote na maoni yao ili watu wawe na amani katika mioyo Yao, Hataki watu wajaze hasira na chuki katika mioyo Yao, Hataki watu wavimbe vifua vyao kwa vinyongo Bali anataka wazungunze kwa heshima, staha, uungwana, busara, upendo,uzalendo wa yale yaliyo ndani Yao na wanayofikiri kuwa yanaweza kuwa na mchango katika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu.

Ndio maana nasema kwa namna Rais Samia anavyokubalika na watu wote wa makabila yote,wa vyama vyote,Dini zote,Rika zote ,jinsia zote, makabila yote, hakika Anastahili kuitwa mama Wa Taifa letu. Anastahili na sioni Cha kuwa kikwazo ambacho unaweza kusema hiki kinamnyima fursa hiyo. Anastahili kwa kuwa ameonyesha uzalendo alio nao ndani ya moyo wake ambao muda wote amaelitaguliza mbele Taifa letu.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Uchawa unakusaidia nini? Wacha nature ifanye kazi yake
 
Bila kubadili mfumo wa UTAWALA wa nchi hii, haya yote ni danganyatoto tu.
Roma haikujengwa kwa siku moja, Serikali ya mama yetu mpendwa mama Samia inaendelea kufanyia kazi kimoja baada ya kingine kwa majadiliano na wdau wote kwa mstakabari Bora wa Taifa letu
 
Back
Top Bottom