Rais Samia aitwe na kutambuliwa kama Mama wa Taifa

Umefanya vizuri kuweka namba, tuombe Mungu impendeze Rais.
 
Unampaka mama mafuta kwa mgongo wa chupa
Kazi aliyoifanya mh Rais haihitaji kupakwa mafuta maana inajionyesha yenyewe kwa yeyote mwenye macho,hata kipofu anaguswa na kazi za mh rais, Kila utakako kwenda unakuta mh Rais ameweka mkono wake ,unakuta mh Rais amewekeza pesa kuwawezesha watanzania kupata huduma karibu yao,unakuta mh Rais amegusa maisha ya watanzania,unakuta mh Rais ameleta Tavasamua ndani ya Mioyo ya watanzania kwa kuwasaidia Kama alivyofanya kwa wakulima kwa kutoa mabillioni ya Ruzuku na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni
 
Mwl. Nyerere aliitwa Baba wa Taifa kwasababu aliiongoza Tanganyika kupata Uhuru na baadae kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar kupata Tanzania. George Washington aliyaongoza majimbo 13 ya mwanzo kutengeneza United States of America ma ndio maana anaitwa Baba wa Taifa la Marekani. Chairman Mao aliianzisha The Today China!

Mama "yako" unataka aitwe Mama wa Taifa kwa lipi?
 
Umerogwa wewe. Uzuri naskia huko kwenye hotuba yake bi chau kakiri kuwa na machawa wake, kina nyie
 
Hilo halina mpinzani Rais Samia Suluhu anaupiga mwingi kila sekta ila hili la leo ametuletea watanzania matumaini mapya kweli Tanzania ni salama na Samia
 
Ameliongoza Taifa kujenga umoja wa kitaifa na kuliunganisha Taifa mpaka kufikia hatua ya kuzungumza lugha moja pasipo kujari itikadi za kisiasa au Dini au kabila
 
Utopolo mtupu na kujikomba. Mama wa taifa ni Afrika.
 
Rais wetu mpendwa Ni mama Wa Taifa kwa namna alivyochapa kazi ndani ya muda mfupi
Huna hoja zaidi ya kujikomba. Au wewe ni Yusuf Makamba au Kinana? Kama una uhaba wa mama si Mama Maria yupo? Au hujui historia ya taifa lako
 
Mi
Huna hoja zaidi ya kujikomba. Au wewe ni Yusuf Makamba au Kinana? Kama una uhaba wa mama si Mama Maria yupo? Au hujui historia ya taifa lako
Mimi sijikombi Bali naeleza ukweli ambao kwa Sasa watanzania Wana uona na kukubali kuwa Rais Samia amefanya kazi ambayo kila mtu anashangaa namna alivyo tekeleza miradi mikubwa ndani ya muda mfupi
 
Rubbish. Bibi PhD hataki chawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…