Rais Samia aitwe na kutambuliwa kama Mama wa Taifa

Mimi Ni mkulima na kilimo ndio kinachonifanya niishi kwa kujipatia chakula
Bei ya mbolea na Pembejeo vipi iko rafiki kwa wakulima? Huko uliko mkukima wewe?

Na bei ya mazao yao huko uliko vipi iko rafiki kwa wakulima? Ukiwemo wewe?

Soko la mazao yao wakulima wenzio huko uliko liko vizuri kwa wakulima huko uliko wewe ukiwa mkulima?
 

Kwani wakati mikutano inazuiliwa Nani alikuwa kaimu Rais.?
 
Mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Hana Deni kwetu wakulima tunalomdai mpaka muda huu maana kazi aliyotufanyia ninkubwa ambayo imeachwa Alama ya furaha katika mioyo yetu,Utolewaji wa Ruzuku ya Billion Mia moja hamsini katika mbolea ilipelekea Bei ya mbolea sokoni kushuka Bei,mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu,Hatua hiyo ilileta shangwe Nderemo na Vifijo kwetu wakulima na kumshukuru Sana Rais wetu kwa kutujali wakulima.

Ukija suala la Bei ya mazao yetu nalo lilikuwa Ni zuri Sana msimu uliopita Tena tangia wakati wa mavuno mkulima alipata Bei ya mazao yake kwa Bei nzuri na hivyo kumfanya kufaidika na jasho lake,Tofauti na miaka mingine ambapo walio kimvulini ndio walifaidika na jasho la mkulima na kumuacha mkulima akiwa mbavu tupu kwa kukondeshwa na jembe analolibeba mabegani muda wote huku akinyeshewa na mvua nakupigwa jua
 
Sijapaniki bali nimeuliza ikiwa huyo ni mama yako, naomba majibu tafadhali
Ndio ni mama yangu na Rais wangu kwa kuwa umri wake Ni sawa na wa mama yangu. Hata mama yako Kama umri wake unaelekeana na wa mama yangu Naye pia nitamwita MAMA.Hiyi ndio heshima ya kiafrika kwa mtu aliyepata malezi Bora ya wazazi wake na aliyekuwa katika maadili mazuri yasiyo ya kihuni kihuni
 
Makamu wa Rais
Rais wetu alaumiwe na kukosolewa kwa Yale yote yanayotendeka na kufanyika katika uongozi wake akiwa Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,Asibebeshwe lawama zisizo mhusu
 

Rubbish
 
How old are you?
 
Rais wetu alaumiwe na kukosolewa kwa Yale yote yanayotendeka na kufanyika katika uongozi wake akiwa Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,Asibebeshwe lawama zisizo mhusu

Umeelewa swali?
 
Huyu anapaswa kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa ikibidi kunyongwa kwa mateso anayowapatia watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…