Mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Hana Deni kwetu wakulima tunalomdai mpaka muda huu maana kazi aliyotufanyia ninkubwa ambayo imeachwa Alama ya furaha katika mioyo yetu,Utolewaji wa Ruzuku ya Billion Mia moja hamsini katika mbolea ilipelekea Bei ya mbolea sokoni kushuka Bei,mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu,Hatua hiyo ilileta shangwe Nderemo na Vifijo kwetu wakulima na kumshukuru Sana Rais wetu kwa kutujali wakulima.
Ukija suala la Bei ya mazao yetu nalo lilikuwa Ni zuri Sana msimu uliopita Tena tangia wakati wa mavuno mkulima alipata Bei ya mazao yake kwa Bei nzuri na hivyo kumfanya kufaidika na jasho lake,Tofauti na miaka mingine ambapo walio kimvulini ndio walifaidika na jasho la mkulima na kumuacha mkulima akiwa mbavu tupu kwa kukondeshwa na jembe analolibeba mabegani muda wote huku akinyeshewa na mvua nakupigwa jua