Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Sawa mkiwa mnatafuta kura hizo shida zenu za kura muwaambie ambao mnasikiliza
Hakuna hata kura zinzotafutwa, huwa zipo tu na wanaozihesabu huwa ndio waamuzi hasa wa kila kitu[emoji16]
 
Kama hawezi sikiliza wananchi basi asingesimama labda anahasira kwa kadi kurudishwa na kuendeleankurudishwa. Asichojua anawakati mgumu kwakua mtangulizi wake alionyesha njia tofauti. Kama leo hawezi wasikiliza basi na kwenye kampeni asiwafuate watu watakua na jambo lao
 
Kuwa rais wa watu ni pamoja na kuwasikiliza wananchi wako shida zao. Wabunge wapo ila hawana rekodi ya kusikiliza shida za mtu mmojamoja. Rais angeiga tu style ya mtangulizi wake alivyoonekana kuwajali wanyonge
Hiyo style ya kutatau matatizo ya raia mmoja mmoja ni mbovu sana na ya kijima.
Wananchi wenyewe wanaopewa microphone mbele ya Rais huwa wanazungumzia zaidi shida zao binafsi, sio hata mambo ya jimbo lao au taifa kwa ujumla.
 
Huwezi kumpangia Rais mahali pa kusimama,
Wazururaji wenyewe wanasimama barabarani popote, itakuwa Rais wa nchi.
Kama hawezi sikiliza wananchi basi asingesimama labda anahasira kwa kadi kurudishwa na kuendeleankurudishwa. Asichojua anawakati mgumu kwakua mtangulizi wake alionyesha njia tofauti. Kama leo hawezi wasikiliza basi na kwenye kampeni asiwafuate watu watakua na jambo lao
 
Hizi itifaki zinamfanya rais asijue kinachoendelea on the ground... viongozi hawawezi kumfikishia vitu negative mara moja moja sio mbaya kusikiliza raia ....
Sio hata itifaki, ni common sense tu.
Pia Rais anajua matatizo yote yanayowakabili raia wa nchi hii, wala hata hahitaji kuambiwa na watu.
 
Na wakati wa kuomba kura basi amtume huyohuyo Mbunge tusimuone huku kwetu maana inaonekana shida zetu hazimuhusu yeye. Sijui tumepata Rais wa aina gani huyu ambaye hataki hata kufahamu changamoto za raia wake. It's very hectic kwa kweli
 
Hapana, Rais anatakiwa ashughulike na mambo ya kitaifa. Huyo raia unaweza kukuta analalamikia kesi ya mirathi ya familia yao au kucheleweshwa mshahara kazini kwake.
Alisimama kuFanya nn? Na kusalimia awe anasalimia kwenye tv/ radio ya taifa! Rais sio sawa kusalimia watu barabarani
 
Na hili nalo muende mkalitazame
Screenshot_20230914-231731.jpg
 
Kuzaliwa kwenye familia ya mwarabu, mboga 10 na kadikodiko hawezi kusikiliza shida zenu. Akiona wananchi hasa watanganyika anahisi kichefuchefu
 
Anaogopa
Rais Samia leo September akiwa mkoani Mtwara alisimamisha msafara wake kuongea na wananchi wa eneo hilo. Moja wananchi hao aliomba kuongea jambo ambapo Rais alimwambia mambo ni mengi na Tanzania ni kubwa.

Rais Samia alimtaka mwananchi huyo ampatie jambo lake mbunge kisha amfikishie Rais au wasaidizi wake.

Mwaka 2017 Rais Magufuli akiwa anaelekea Mtwara alisimamishwa Somanga na mwananchi aliyeelezea changamoto ya zahanati katika eneo hilo kutokamilika kwa miaka mingi. Rais Magufuli alichangia na kuamrisha ikamilike.

Alipopita tena barabara hiyo miaka 3 baadae mwananchi huyo alimzawadia jogoo kama shukrani ya kutimiza ahadi ya kufanyia kazi dukuduku lake na Magufuli alimsubiri mpaka alipomkamatia na kumpa. Alipofariki, mwananchi huyo alifunga safari kumzika Rais Magufuli mwaka 2021.

View attachment 2750834Anaogopa swali la Bamdari. Hana uhakika na majibu au vipi?​
 
Ni kweli Rais hawezi kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja, itakuwa jau sana .... mwingine kapigwa na mumewe anataka kesi apeleke kwa Rais, tutamaliza saa ngapi?
Si alimchagua kama ubavu wa Jpm? Kukataa kupokea ujumbe wa Ana kwa Ana ni istana ya wasiwasi au hukujiandaa.
UKIWA MCHAFU HATA WATOTO WAKITAKA KUKUULIZA LAZIMA UKATAE
 
Hiyo style ya kutatau matatizo ya raia mmoja mmoja ni mbovu sana na ya kijima.
Wananchi wenyewe wanaopewa microphone mbele ya Rais huwa wanazungumzia zaidi shida zao binafsi, sio hata mambo ya jimbo lao au taifa kwa ujumla.
kimsingi hawana elimu na hawajui itifaki ya viongozi wa kitaifa. Marais wengine hawakufanya hivyo ila wanapofanya ku solve tatizo la mtu binafsi hufanya hivyo kisiasa tu. Ni mchezo wa kisiasa kujifanya uko karibu na wananchi wa chini mmoja mmoja.
 
Umejuaje kama huyo mwananchi alitaka kuuliza swali binafsi, haya tuchukulie suala binafsi labda mwananchi kaibiwa mifugo yake...Rais si anampasia DC kulishughulikia, inakuwa ni agizo sasa la Rais kwasabb hawa viongozi wetu huku mawilayani saa zingine wanapenda sana ubwanyenye wanachelewa kuchukua hatua!.
 
Back
Top Bottom