Rais Samia akikupa mualiko Ikulu wa dakika 5 utamshauri nini kama kijana wa kitanzania?

Rais Samia akikupa mualiko Ikulu wa dakika 5 utamshauri nini kama kijana wa kitanzania?

Atuangalie na sisi wasomi tusio na ajira kama akishindwa kutuajiri basi atukabidhi ardhi tijikite kwenye kilimo watupe mitaji pia atuweke miundo mbinu wezeshi pamoja na kutuandalia soko la nje. Tulime mazao ya biashara
vp umejisalili Ajira portal na Taesa?

hukuomba BBT ?
 
Mimi nitamshauri yafuatayo kiongozi
1.Uwepo wa NISHATI ya UMEME wa uhakika, hili ataweza kwa kupunguza kasi ya ujenzi wa SGR hasa toka Tabora kwenda huko kwingine,hela yake apeleke Stigler hydropower

2.Atupatie KATIBA MPYA ILIYO BORA na TUME HURU ya Uchaguzi

3.Aingilie utendaji wa huu mradi wa mabasi yaendayo haraka,DART, kwani Mawaziri wake wameshindwa kabisa...Na namna bora ni kuhusisha SEKTA BINAFSI..Dar ndio Tanzania Mama yetu mpendwa!
 
ushauri mzuri sana chief
 
Ahakikishe nchi inapata university teaching hospital.
 
Awamu ya sita ya mama Samia tumeona mengi yakifanyika ikiwemo utekelezaji wa miradi ya umwangiliaji ya kilimo, BBT, Ruzuku ya mbolea, Afya, Ajira, Veta, kupandishwa madaraja kwa watumishi nk

Lakini pia zipo changamoto kadha wa kadha ambazo watanzania wanatamani wamfikishie Rais wao, nao wajione ni sehemu ya watanzania wanaofaidi matunda ya nchi hii!

Rais amekupa dakika tano tu umpongeze na umshauri kipi kiboreshwe ama kiongezeke kwenye utawala wake ili kila mtu ajivunie kuwa mtanzania, utazungumza nini?
Nitamshauri kuwa viongozi wako wengi wanatembea Bara la ulaya na wanaona usafiri wa umma ni matreni ya mijini ambayo akinunua ma 4 tu yanatosha kuhudumia mkoa wa Dsm lakini haya mabasi ambayo yana nunuliwa kila mwezi yana kufa hawaoni kuwa ni hasara na nikiro kwa wana nchi.

Kupitia nafasi hii namuomba mama aangalie jinsi anvyo hukumiwa kwenye mabasi ya mwendo kasi, kila baada ya mweizi 6 mabasi yanakufa yanatakiwa yanunuliwe mengine hii ni hujuma ya waaiwazi.ili daladala za matrafiki za mapolice za viongozi mbalimbali zifanye kazi.

Ninacho shauri
Anunue treni za mijini kama zile za ulaya zipite kuanzia kariakoo kwenda kimara na sio mabasi.
 
Awamu ya sita ya mama Samia tumeona mengi yakifanyika ikiwemo utekelezaji wa miradi ya umwangiliaji ya kilimo, BBT, Ruzuku ya mbolea, Afya, Ajira, Veta, kupandishwa madaraja kwa watumishi nk

Lakini pia zipo changamoto kadha wa kadha ambazo watanzania wanatamani wamfikishie Rais wao, nao wajione ni sehemu ya watanzania wanaofaidi matunda ya nchi hii!

Rais amekupa dakika tano tu umpongeze na umshauri kipi kiboreshwe ama kiongezeke kwenye utawala wake ili kila mtu ajivunie kuwa mtanzania, utazungumza nini?
Alianza kwa kutuonesha kumbe hakua na magufuli kitu kimoja. Jaribio lake kufungua milango kwa ubeberu limepingwa kwa nguvu sana hadi inaonekana kwa yeye kuanza kurudi kwenye njia ya kizalendo. Binafsi ningemshauri kwamba njia sahihi ni kufuata njia ya kizalendo. Kulenga kutegemea nguvu ya ndani na kujenga usawa kwa raia.
Ushauri wa pili ajue imani kwa njia ya kimaguli kwa watanzania ni kubwa sana. 2025 ahakikishe taifa linampata mtu mwenye mwelekeo wa sera za kimagufuli ambaye siye yeye maana ameshapoteza imani ya wazalendo ambao ndio hazina kujenga nchi ya kujitegemea haki na uchumi imara.
 
Asambaze UMEME vijijini, alime barabara za vijijini, apunguze MISHAHARA ya Wabunge aongeze MISHAHARA ya Walimu. Asambaze maji vijijini. Kila kitongoji kipate UMEME na serikali ihakikishe kila nyumba ya mtu Ina umeme. Sehemu ambako umeme kufika ni changamoto serikali iwagawie watu Solar.
 
Back
Top Bottom