Rais Samia akipokea Kombe la Dunia, Ikulu, Dar es Salaam Mei 31, 2022

Fursa zipi hizo?

Achaneni na mapambio yasiyo na jinsia!
 
Wewe ndio unauelewa mdogo mkuu

Ile ilikuwa kada ya siasa
Hii ni kada ya michezo

Soma kanuni za FIFA au sera zake halafu rudi tena

Siasa na Michezo haziingiliwi na serikali au kiashiria chochote kutoka serikalini

Ngoja niwatagi wakenya mwakani hawashiriki mashindano ya africa cup of nations kwa sababu za kuchanganya siasa na Michezo
 
Tujikite kuji-advetise kwenye kombe la Dunia hasa final, UEFA Champion league final, Wimbledon, French, Australia, US tennis competitions. Pia Major golf tournaments including masters, expos etc.
 
Reactions: Cyb
Sujui ni lini na sisi tutalibeba Kombe la Dunia.
Kwanza tulitafute la shirikisho hapa Africa ! Labda Coastal Union siku moja wanaweza kulileta maana Hao wengine wanaoitwa majabali ya soka Nchini wote mpaka sasa wameshindwa kulileta !!!
 
Naamini hata wewe tukio limekuvutia, kumbuka CCM watakuwa wapinzani siku moja sijui utakuwa upande gani wakati huo.
 
Kupokea ndege na pia kupokea Kombe la Dunia zote mbili sio ushamba.
Ila ushamba ni kupokea kila ndege inayokuwa delivered, tena kwa sherehe ya kitaifa..
Mara moja inatosha..
 
Kama watu watapinga hadi jambo hili nitaamini sio siasa bali ni wivu na chuki binafsi kwa SSH..
 
Hiyo ni kazi ya waziri wa michezo, rais kwenda kwa hayo ni kutowajibika. Kuna kazi ambazo zinamhitaji hazifanyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…