Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
=======
Rais Samia akipokea Kombe
Ndungu Waalikwa mabibi na mabwana, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kazi iendelee,
Leo tunafurahi, sana na tunasherehekea kuliona kombe la Dunia, ambalo limepita hapa kwetu kabla ya kwenda Qatar, Pia tunafurahoi kuwaona wageni waliokuja nalo, pia kumuona mchezaji wa zamani Juliono Bereti kwamba leo amefika Tanzania vijana watafurahi kumuona mchezaji huyu nguli wa zamani.
Kesho kombe hili litakuwa pale uwanja wa Mkapa, ila nitoe Idhari, kwani nimesikia mmesema wanayo nafasi ya kupiga nalo picha Umma utakaomimika pale kutaka kupiga hizo picha naomba kuwepo na ratiba nzuri itakayofanyamambo yaende vizuri pale.
Lakini pia kombe hili linakwenda kugombaniwa kule Qatar ingawa hatumo ila tumo katika nchi ambazo zimepelekewa kwenda kuliona, japo kuna wengine wakipata nafasi watakwenda Qatar kwenda kuliona likigombaniwa. Nimejulishwa kuwa kombe hili litazungushwa kwenye nchi 9, 5 zitashiriki na 4 hatutashiriki, wengine wanashiriki ila ni heshima kwetu kuwa tumeletewa kuliona hii ni heshima kubwa kwetu.
Nimeelezwa kuwa hii ni mara ya nne Kombe hili linaletwa kwetu mara ya mwisho ni 2014 ambapo Rais wetu Hayati Benjamini Mkapa alilipokea kwa hiyo leo miaka kadhaa imepita na leo tunalipokea na tunaliona sisi kabla ya waQatar kuliona.
Lakini Kombe hili kuja kwetu kwa fursa zinazoweza kupatikana lakini kubwa kwetu lina mchango wa kiuchumi na kijamii lakini pia ni kuitangaza nchi yetu na Cocacola wamelibeba hilo na kwamba mtaendelea kulibeba kombe hili na kuitangaza nchi yetu na kombe hili liwe fursa kwetu kwani dada zetu wametoka majumbani wamewaacha viongozi wetu majumbani kuja kulipokea kombe hili halafu lipite tu hivihivi bila faida haiwezekani kwa hiyo tuitumie fursa hii na kuitangaza nchi yetu katika ramani ya dunia ambayo imejaa kila aina ya ushindani.
Nitumie fursa hii kwa wizara ya michezo kwa kuendelea kushirikiana na kombe la mpira wa miguu Tanzania kwa kuendelea kutumia mchezo wa mpira kuitangaza nchi yetu, Juzi niliona walikuwa pale daraja la Tanzanite na ule ulikuwa ni ubunifu kwani sasa ulimwenguunajua Tanzania wana daraja linaitwa Tanzanite na uzuri taa zilikuwa zinawaka na hivyo dunia imejua vivutio zaidi.
Lakini pia Kuitangaza nchi yetu na kuisemea mazuri na kujipanga vizuri kutumia fursa vizuri kila zinapojitokeza kama kutoa huduama au kufanya biashara, naposema huduma ni huduma halali na si watokee wale wengine kwenda kupanga kutoa huduma kule wale wasichana tutawakamata na kupigana nao vizuri, lakini pia tulitunze vizuri kombe hili lifike salama sio lifike huko na vidotidoti.