Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Kiwango cha ongezeko la mshahara halijatajwa kwenye hiyo barua ila Rais ameridhia mapendekezo ya nyongeza.

Hiyo 23.3% ni ongezeko la kima cha chini cha mshahara.

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa,JK aliongeza kwa 30% mwaka 2012 hicho kima cha chini cha mshahara kutoka 150K to 180K.
 
Wamepigwa wameekewa adi decimal hii nchi iko siku itapigwa Bei ,na kukopa wamekopa Tena usd billion kadhaa
 
Ww sukuma gang...waache watumishi wafaidi uongozi shupavu wa mama
Sawa endeleza ushabiki lakn si utarudi mtaani Hali ilivyo hao waliopo serikalin tunazungumzia 70% ni wazee wa miak ya 60 ,70 na 80 Sasa wee uliemaliz chuo jana anakuajili Nani?
 
Vingaravyo si Dhahabu tu Shaba pia huhilibu 🤌
 
Chadema mlikuwa mnamsifia Kenyatta kuongeza asilimia 15 mkatukana CCM na Raisi Mama Samia mbona siwaoni njooni huku mumsifie Raisi Mama Samia

Mumekalia kusifia nje tu maruhuni nyie msio na uzalendo.Mama Samia kavunja rekodi ya Kenyata mliyekuwa mkimsifia hadi mkawa mnajisikia haja kubwa kwa kumsifia
Shukuru matusi hayo wewe!
 
Mkuu Kuna watu wanasema et 23.3% ni kwa wale tu wa kima Cha chini.lakini Mimi ninavyojua ni kama wewe hivihivi,basic salary inaongezeka kwa 23.3% kwa wote ila take home itapungua kulingana na Kodi yako.
Nyongeza ya msharaha ikiwa kwenye mshahara ni kwa wote.
Anayelipwa 400,000 itaongezeka 23.3%
Na anayelipwa mil 6 itaongezeka 23.3%

Ila kwenye Kodi, huyo wa mil 6 Kodi yake inaweza kumega hiyo nyongeza hadi kwa 40%
 
Kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania , nyongeza ya mshahara wa wafanyakazi kila mwaka ni takwa la kisheria , limo ndani ya Katiba ya Nchi ambayo kila kiongozi mwenye akili timamu anapaswa kuifuata , hii ni kwa sababu aliapa kuilinda na kuitii .

Kwa Hiyo kwa Mama kuongeza mshahara kwa hizo 23.3 % si ajabu na wala si jambo la kushangaza , Kwa vile amefuata matakwa ya Katiba ya nchi kama inavyomuelekeza , nyongeza ya mshahara si mapendo ya Rais , amelazimishwa ndani ya Katiba , hakuna haja ya kumsifia as if Mshahara huo ameongeza kutoka nyumbani kwake , sana sana apongezwe kwa kuanza kuijua vizuri Katiba ya nchi .

Ikumbukwe kwamba sipingi nyongeza ya mshahara kwa Wafanyakazi wa Tanzania makapuku , waliosomeshwa namba kwa miaka 7 , isipokuwa nanyoosha tu maelezo kwamba KUPANDA KWA MSHAHARA SI HISANI YA RAIS , BALI NI MATAKWA YA KATIBA YA NCHI .

Naomba kuwasilisha .
 
Naomba nitofautiane na wewe kimawazo kwanza nyongeza ya mishahara Kila mwaka siyo takwa la kisheria hilo uelewe isipokuwa annual salary increament ndiyo ipo kisheria kwa Kila mtumishi ndiyo maana ipo Kwenye barua ya Kila mtumishi ya ajira au kupanda daraja.Nirudi Kwenye hoja yako ya kumsifia Rais(mama) Kwenye hili nakujibu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Mimi nitamsifu na kumpongeza mhe Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa 23.3%, kumlinganisha na mtangulizi wake ambaye aliwakalisha watumishi wa umma bila nyongeza ya mishahara kwa zaidi ya miaka sita.Mimi nitaendelea kumsifu na kumpongeza mhe Rais kwa kusikiliza kilio Cha watumishi wa umma hata kama ni ujinga wacha niwe mjinga.
 
What is annual Salary increament ?
 
Back
Top Bottom