Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Watu kama Dangote wanahitaji serikali zenye watu wenye akili sana na ujuzi wa namna wafanyabiashara wakubwa walivyo. I bet if we have that brain NOW
Je hali ilikuwaje wakati wa shujaa?
 
Kama Monopoly ambayo anapenda Dangote anatuuzia cement bei poa kama ile ya 10,000,(vunja bei) safi kabisa...sasa sie wananchi huyo ndo afadhali atuokoe kuliko maviwanda hayo mengine,yanayotukomoa kwa bei za cement za juu kila uchwao.... kazi iendelee yaVunja bei....
Shida kubwa ya Dangote ni mtu anaeamini in monopoly. Sehemu zote anapowekeza huwa ana bad reputation ya ku corrupt viongozi wa kisiasa ili kuua competition nahisi ndio maana hawakuwezana na mwendazake.
 
Huyu mjukuu wa aliko Dan tata afanye mchakato cement irudi elf 10 Ili wanyonge tuachane na nyumba za nyasi
Mkuu, washindani wake wenye viwanda vya saruji hapa nchini wataungana na kumpiga vita vya chini chini Dangote kama walivyo fanya mwaka juzi - kuna mambo ya wa ajabu nchi hii yenye lengo la kukwamisha wawekezaji wenye uwezo mkubwa kimtaji - haya mambo yakusema eti Taifa linaruhusu biashara uria ni hiyo ni danganya toto - waulizeni WavietNam walipo kuja na pendekezo la kushusha gharama za ununuzi wa bundle za data na voice - kampuni kubwa za simu nchini ziliwatisha tisha WavietNam wa watu mpaka wakaingia laini - sikuona TCRA wala inaingilia kati ku-support juhudi za HaloTel kuwapatia wananchi unafuu wa gharama za mawasiliano mpaka tunashindwa na nchi kama Rwanda.
 
,,Kila kitu kimebadilika na hakikika wawekezaji wataludi,,tusubiri tuone
 
Pengine hufahamu effect ya monopoly. Once akiwa ndie pekee anae endesha biashara ya cement tegemea kuwa ata control bei. Mlaji siku zote ana fadikia kwenye soko lenye ushindani. Mwogope mtu mwenye imani ya monopoly kama ukoma.
 
Kwa hiyo yeye anataka apendelewe zaidi wote, haisee hapo kazi ipo ,NI VYEMA MAKAMPUNI YOTE YA SARUJI YAKAPATIWA EQUAL AND FAIR RIGHTS,KUSIWE NA WA KUDEKA ZAIDI,BUT KWA UFAHAMU WANGU NIGERIANS ARE SO STUBBORN PEOPLES,AKILI YAO INAWATUMAGA LAZIMA WAKUZIDI KETE,NDIO ANAONA SAFI KABISA HII NDIO NATURE YAO HAWA JAMAA,HAKUNA CHA KIJANA AU MZEE WOTE NI WAMOJA,TO BE AHEAD IN EACH STEPS.
 
Mwendazake hayati rais John Pombe Joseph Magufuli, mwenyewe alilalamikia watu wake serikalini kwa kukwamisha malengo ya Dangote kule kusini:

Ahsante sana Bagamoyo,
Kweli teknologia haiongopi, ndio hiki nimekizungumzia, na hapo nimesikia hata huo mpango wa kujenga kiwanda cha mbolea ulikuwa toka hicho kipingi cha Magufuli.

wamlaum kwa mambo mengine lakini haki yake apewa,

kwangu mimi Magufuli amefanya mambo ambayo watanzania tuliyalilia muda mrefu.
 
Sasa figisu za nini kama kodi anawalipa? muacheni afanye kazi kwa amani, hii mikutano ya aina hii ndio inafungua njia kwa wawekezaji wengine kuwa na amani ya kuja kuwekeza Tanzania.
Awamu zote Tanzania imekuwa na wawekezaji na matokeo yamekuwa hasi/chaya kuligana na msimamo/maono ya Rais aliyeko madarakani pale Serikali:-
[emoji830]︎ Awamu ya Kwanza - Ujamaa: utaifishaji na umiliki wa njia kuu za uchumi, palipo stahili ushirikiano na wawekezaji;
[emoji830]︎ Awamu ya Pili - Rukhsa: kufanya chochote/lolote lakini hapukuwa na uwekezaji wa maana zaidi ya kuibua Misheni Town;
[emoji830]︎ Awamu ya Tatu - Utawala Bora: ubinafsishaji wa njia kuu za uchumi, wawekezaji wakabadili km viwanda kuwa maghala ya bidhaa zao kutoka nje;
[emoji830]︎ Awamu ya Nne - Ari mpya na Kasi mpya: Tanzania yageuzwa shamba la bibi. Tunashuhudia uwekezaji kwenye sekta ya anasa km mahoteli, majumba ya starehe, na "shopping malls";
[emoji830]︎ Awamu ya Tano - Hapa Kazi tu: ujenzi wa miundo mbinu na kuboresha huduma za jamii kwa fedha za ndani. Kufanikisha hilo mianya ya kukwepa kodi inazibwa na baadhi ya wafanya biashara wanazifunga na kuzihamishia nje ya nchi; na
☆ Awamu ya Sita - Kazi inaendelea: Diplomasia ya uchumi kushawishi wawekezaji kutoka nje mradi hawaifanyi Tanzania shamba la bibi tena.
 
Safi,
Na zaidi hapo aliyekuwa anatupeleka pazuri kama taifa ni mwendazake kwa kufuata nini huyo wa awamu ya kwanza alipotaka kutupeleka,

ni matumaini yetu Watanzania Mama ataendeleza ya mtangulizi wake
 
Ukichunguza sana, Mwendazake wala hakuwa na asili ya Tanzania.
Wanaosema msukuma nakataa kabisa, hana hata dalili ya usukuma ndani yake!
KABISA mkuu. Haowezekani Mtanzania asili uwe na Roho Ile. Yaani hata Wa Tanzania walowezi humu nchi ni wengi tu na walikuwa au wana vyeo lakini si kwa hali Ile. Na Wasukuma nijuavyo si wa tabia is Ile kabisa. Kuna wakati iliubuliwa miaka kadhaa iliyopita kuhusu asili yake? Babu yake migrated to Tz and his father was born in Tanzania but he claimed that his father acquired Tz Citizenship??? No wonder
 
Shukrani sana Mkuu
 
Tutengeneze sera za kudumu kwenye uwekezaji siyo akija mwingine ana haribu na kukimbiza wawekezaji
Umenena vema kabisa. Sera za Uwekezaji inatakiwa iwe ni mipango ya Kimkakati ya Ki-Taifa tena ya muda mrefu. Sera ya Uwekezaji haipaswi kubadilishwa pale Kiongozi mmoja anapoondoka na kubalisha uongozi wa Kitaifa. Ndio maana Uwekezaji Tanzania umekuwa ukisuasua mno kwa kile Wawekezajia wanacho kilalamikia kuwa "luck of seriousness and vision" ya viongozi wa Tanzania kwenye masuala mazima ya Uwekezaji mkubwa na wa kimkakakati.
 
Majukumu ya Rais ni nini hapo?

Hebu nambie Samia na Dangote wamekutana kufanya nini?

Dangote amealikwa Ikulu kuja kufanya nini?
Rais ndiye balozi/mwanadiplomasia namba 1 wa nchi, Moja ya jukumu lake kubwa ni kuunganisha nchi na jumuiya ya kimataifa. Siyo kila kitu unamtuma FM or VP, uzito wa kuwepo wewe kama Rais ni mkubwa kuliko kutuma watu
 
Rais ndiye balozi/mwanadiplomasia namba 1 wa nchi, Moja ya jukumu lake kubwa ni kuunganisha nchi na jumuiya ya kimataifa. Siyo kila kitu unamtuma FM or VP, uzito wa kuwepo wewe kama Rais ni mkubwa kuliko kutuma watu
Jibu swali.

Samia na Dangote wamefanya nini, wameamua nini jana ????

Dangote alipewa presidential audience kuja kufanya nini Ikulu ?
 
Haya ndiyo majukumu ya Rais sasa, siyo kutafuta cheap popularity kwa watu wenye upeo finyu (Machinga, bodaboda, mamantilie na wauza nyanya wa Dumila), matokeo yake unaenda hadi kuzindua vyoo na kuwaambia watu waache mavi yao nyumbani. Hongera Mother

Mtu kuwa wa kipato cha chini haina maana ana upeo finyu. Wewe ndo umeonyesha kuwa na upeo finyu.
 
Tutengeneze sera za kudumu kwenye uwekezaji siyo akija mwingine ana haribu na kukimbiza wawekezaji
Mkuu Babati kwa kuwa una chuki na uongozi wa CCM badala ya kuwa mchambuzi, kwa maslahi mapana ya Taifa, hujapenda kusoma na/au kufuatilia utekelezaji wa Ilani zake za Uchaguzi ambazo kimsingi ni mikakati ya kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa (Development Vision 2025).

Moja ya mikakati iliyomo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2025 kuhusu Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi ni Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango stahiki katika maendeleo ya nchi yetu.

Serikali zote za CCM zimekuwa zikifanya hivyo tofauti imekuwa katika kutafsiri Ilani zake na kusimamia utekelezaji.
 
Hongera mama Rais wetu Samia Suluhu Hassan, hakika Mama Mungu akulide daima, ww ni Nuru ya Taifa letu 🙏
 
Ba ndio sababu ya mkuu wa mkoa alipangiwa kazi nyingine
 
Ni kweli kabisa mkuu kama hili la kutuletea wasiojulikana na kuanza kuteka watu ovyo naona ulilitamani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…